Msaada: Kuagiza nguo online toka China kupitia Alibaba

Mm nataman kununua nguo mitandaoni hasa from dubai baibuiz abayaz n the likes sema natafuta kampuni resonabo zinazotengeneza nguo ili ninunue on cheap ww unanunuaga wap mkuu
 
Wewe jamaaa hukuwahi kabisa kuagiza au kufanya biashara na hawa jamaaa,mm mwak jana nilitaka DISPLAY YA CM ,nika join kwa email,unachagua bidhaa then unakabidhiwa mtu ambaye uhusika na bidhaaa hiyo tena kwa namba ya cm,utachat nao kwa kutumia fb,whatsapp na mengine,hawa jamaaa hawana longolong tena ndan ya siku saba mzigo wako umefika hapa bongo.
NB:KAMA HUJUI AU HUKUWAHI CHA KUAGIZA HATA KIKOMBE ACHA UNAFIKI,NGOZ NYEUSI NYIE ACHENI UNAFIKI,HUO USHAMBA
 
Jamaaaa wako poa sna,ukitaka hata kuulizia tu mm nipo tayari kukupa namba yao kuwauliza na nafanya nao biashara sna hawa jmaaa.
Waafrica weng wetu waongo yaan ilimradi nae aonekane anajua kumbe hata jins ya kujoin hajui
 
Naona online vitu vingi wanaweka retail prices
 
Alibaba haina shida itakusaidia kumeet na manufacturer au supplier.
Cha msingi tumia kampuni zenye ofisi tanzania na china wenye huduma za kutuma pesa na kusafirisha mizigo, wao watalipa pesa kwa niaba yako baada ya kupokea mzigo na pesa zako zitakua salama.
Check na Javis international
 

Nadhani unaweza kuagiza kupitia Alibaba na ukapata bidhaa yako ktk Ubora unaoutaka na kwa Uhakika. Alibaba wana Bima ya MUAMALA utakaofanya kupitia Alibaba, kuhusu Ubora unaweza kuwa na mkaguzi ambae atahakikisha kua vigezo VYAKO vimefiki wa ktk hiyo bidhaa.
Kinachosababisha watu kupata hasara Ni kwa kushindwa kufuata taratibu na pia kushindwa kujua bidhaa nzuri inabidi iwe na nini ndani yake! (Specification, details) Karibu kila anaelizwa utakuta alikosea ktk taratibu au hakuweza kufafanua Ubora anaoutaka.
Unaweza kusoma zaidi kutoka Import from China - Buyer's Guide
 
Hata mimi nina idea kama yako mkuu but mimi napendelea women handbags and shoes

Ni wazo zuri. Mimi nilifanikiwa kuanza biashara ya kuuza viatu vya akina mama na watoto, urembo na vipodozi mwaka jana.Bado sijafanikiwa kuagiza nje ya nchi, kwa sasa ninachukua kariakoo.Kwa mazingira nilipo biashara inaenda vizuri.Mara nyingi mzigo nafunga weekend pale kariakoo.Viatu vya akina mama huwa navipata pale mtaa wa Kongo maduka ya wachina na vipodozi pamoja na urembo vinapatikana opposite na kituo cha kuuza mafuta Bigbone.Nimepata uzoefu. wa namna ya kuendesha hii biashara.Nimeweza kubuni mbinu mbalimbali za kuboost mauzo kulingana na mazingira nilipo.Kikubwa nilichojifunza biashara hii inahitaji commitment ya hali ya juu.
 
ALIBABA ni neno la Kiarabu maana yake kwa kiswahili ni MWIZI!!! Kwa hiyo kuwa makini kaka.
Mbona mkuu unafanya conclusion kwa chuki kaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kupitia stori za vjiweni.Una uhakika hao Alibaba ni waarabu?
 
Magufuli afanye mpango atembele posta ya Dsm upande wanapo tuma na kupokea mizigo pale ni jipu lina hitaji mtumbuaji
 
Maneno ya elungata ni sahihi kabisa. Tushawahi kununua bidaa alibaba na unapata bila wasi .si waarabu ni kampuni ya kichina
 
Jamani kama kuna mtu yoyote ambae ana uhakika na ni mzoefu wa kununua bidhaa online afunguke tuachane na story za vijiweni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…