Msaada: Kufanya kazi Jeshini au kuwa raia wa kawaida kipi bora?

Miaka 11 iliyopita baada ya kumaliza chuo niliwahi kuwa na munkari wa kuingia jeshini tena direct kwa kutumia elimi niliyopata kwa kipindi hiko....

Nikamfuata ndugu yangu mmoja mwanajeshi mwenye cheo kiasi nikamuomba ushauri...

Alichonijibu

"Kama unataka kuingia jeshi kwa kuwa unaona ajira ni ngumu lakini moyo wako haukutumi kwenda jeshi acha usiende, na kama umeridhia kuingia kwa moyo wako wote na unaipenda moyoni basi ingia nitakusaidia kila kitu.."

Nikakaa nikawaza kama wiki hivi. Mwisho nikaamua nibaki kitaa nipambane....

Nakushauri achana na mambo ya jeshi kama moyo na dhamira yako haitaki...
 
Thread closed
 
I second you
 
Ngoja nikushauri kitu mdogo wangu tena unisikilize kwa makini sana.

Usiende kwenye kazi ya uaskari kwa sababu huna ajira au usifanye kazi ya uaskari kama sehemu ya kwenda kuzugia utakuja kujuta.

Ila nenda kwenye kazi ya uaskari kama uliipenda tangu zamani na ulikuwa una ndoto hiyo.

Na usifikiri ukiingia kwenye kazi ya uaskari utatoka kirahisi kama watu wanavyoacha kazi kwenye kampuni za kiraia.

Kuna rafiki zangu wengi waliingia kwenye kazi ya uaskari kwa mawazo kama yako wewe hadi sasa hivi miaka 10 imepita bado hawajachomoka.

Tena kuna mmoja huyo yeye alivyoingia kazi ya uaskari baada ya mwaka akawa ameichoka kazi akawa anatoroka anarudi nyumbani basi unaambiwa walikuwa wanamfuata hadi nyumbani kwao wanambeba kinguvu wanamuadhibu kisha wanamrudisha kazini,hadi hii leo miaka zaidi ya 10 imepita bado yuko huko imebidi tu aizoee kazi yake.

Kwa hiyo shida au kukosa kazi isikufanye ukurupuke kwenye maamuzi ambayo sio sahihi.
 
Baki uraiani
 
Shukrani sana nimekupata
 
Ndiyo ninachokipitia sasa, shukrani sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…