Extroverted Introvert
JF-Expert Member
- Aug 18, 2022
- 599
- 1,565
Habarini ndugu zangu,
Kama jina “linavyo-display” hapo juu. Baada ya kuhitimu bachelor’s degree miaka kadhaa iliyopita na kusambaza CV ofisi mbali mbali, hatimaye mapema mwaka jana nilipata nafasi kama “intern” kwenye taasisi ya kiserikali (nalipwa 150,00Tsh kwa mwezi, posho zingine kama za safari na vikao) na ndipo nilipo mpaka wakati huu, na ninavyoandika uzi huu nipo ofisin nimetulia nasubiri muda wa kazi niendelee kuitumikia serikali yangu.
Recently, kuna nafasi imekuja ya kujiunga taasisi ya kijeshi (moja kati ya polisi, zimamoto na magereza) lakini kwa kutumia elimu ya form 4/form 6. Lakini kiuhalisia sina amani kabisa kufanya kazi huku. Napenda kufanya kazi niwe kama raia wa kawaida na kuendelea kutumia maarifa yangu niliyoyapata through my degree’s journey.
After these two scenarios, nimekwama kwenye maamuzi. Kama mnavyojua maisha mtaani magumu ila hatuchoki kutafuta, (1) natamani kuendelea na internship huku nikiendelea kusambaza CV (nafurahia taasisi za kiraia). (2) Natamani niingie huko kwenye “uaskari” ili niepuke hiki kikombe cha maisha magumu huku mtaani (sina amani kufanya sekta hizi). Ushauri tafadhali kwa wale wakongwe na wazoefu kwenye mambo haya ya ajira,
Pia ningetaka kujua je, baada ya kuingia huko kwenye “uaskari” naweza kuhama kama wengine wanavyohama kutoka ofisi moja kwenda nyingine (mfano kutoka uaskari kwenye TMDA, TBS, Halmashauri na taasisi zingine kama hizo)?
Changamoto niliyonayo: siko vizuri kwenye interviews (nimefanya nyingi) lakini naendelea kuji-expose kwenye maongezi mbalimbali na kujifua zaidi ili kutengeneza confidence, kujieleza na kujenga hoja.
Hitimisho: nimeleta uzi humu sababu kuna advisory experts, psychology specialists, HRs na watu wengine wenye uzoefu na mambo/changamoto kama hiyo.
Ahsante.