Msaada kuhusu fixed account

Msaada kuhusu fixed account

Full charge

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2018
Posts
1,678
Reaction score
1,617
Habari za muda huu wakuu,

Mimi ni kijana kama vijana wengine wapambanaji,ila changamoto nayopata kuhusu uhifadhi wa pesa ni kubwa mno.

Nimefungua akaunti benki kadhaa ila nikipata shida kidogo naenda kutoa pesa achilia mbali makato yao hii hali inanifanya pia nitimize malengo kwa muda mrefu.

Moja ya changamoto zinazofanya nitoe pesa benki kwa shida ndogo ni mtu nayeishi nae hawezi kujikaza kama akijua nina pesa.

Sasa wadau naombeni mbinu,sifa na udhaifu wa fixed account ili nikiweka huko basi nikiulizwa pesa najitetea kuwa haiwezi kutoka mpaka limit of time🙏
 
Mkuu katika haya maisha hakuna mtu yeyote anayejali kuhusu wewe.

Kila mtu yupo na wewe kwasababu maalumu na wengi wanakuwa na wewe wakiona una kitu ambacho wanaweza kupata kutoka kwako.

Acha kutumia hisia kufanya maamuzi bali tumia ubongo.

Akiba ni mbegu na ni msingi wa kuyajenga maisha yako.

Thamini akiba yako kuliko jinsi unavyothamini kitu au mtu yoyote.

Akiba yako ndiyo ulinzi wako na ndiyo egemeo lako ukipata changamoto kubwa katika maisha.


Linda akiba yako na kuwa na maamuzi magumu linapokuja kwenye suala la pesa.

Penda sana kutumia haya maneno "SINA" na "HAPANA" na kamwe usiogope mtazamo wa mtu juu yako.

Kama haujanielewa subiri upate shida kubwa kisha uone ni wangapi watakuwa na wewe katika nyakati hizo ngumu.

Hapo ndipo utaelewa umuhimu wa akiba yako na utaanza kuilinda kwa hali na mali.

Kwenye pesa hatufanyi maamuzi kwa kutumia hisia. Upendo kwenye Hela weka pembeni na fanya maamuzi kwa mahesabu na akili.
 
Back
Top Bottom