Msaada kuhusu gharama za fundi kujenga nyumba ya vyumba vitatu kuanzia msingi hadi kwenye beam

Msaada kuhusu gharama za fundi kujenga nyumba ya vyumba vitatu kuanzia msingi hadi kwenye beam

davetz28

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2017
Posts
543
Reaction score
624
Nawasalimu wanajamvi wote,hongereni kwa majukumu ya kujenga taifa. Leo nimekuja kwenu kuomba ushauri ni kipino gani kinatumika kupata bei ya ujenzi wa nyumba?

Nimempata fundi aniinulie boma kuanzia msingi hadi kwenye hatua ya lenta,mahesabu yake aliyopiga ni shs 500 KWA tofari moja gharama itahusu pia kuchimba msimgi na gharama ya kumwaga zege la beam.

Je, wewe ulitumia njia gani kupataa gharama ya ujenzi? Nitashukuru sana lwa mchango wenu wa mawazo.

Baada ya kupiga mahesabu jumla imefika milioni laki saba.
 
Fundi yupi tena? Nataka nipate uzoefu fundi wangu ndio kanipa hayo mahesabu na bado hatujafikia makubaliano..Binafsi naona mahesabu ni makubwa sana.
Upo mkoa gani nikuunge na fundi aliyenijengea. Very affordable huyu jamaa.
 
Kama upo Dar nikupe namba ya fundi najua mtawezana yani ana crue yake kama kuchimba msingi kuanzia kujenga hadi kupaua yupo vizuri na ni affordable.
 
Gharama zinategemea vitu vingi sana, kwa uchache
1.Ukubwa wa Jengo
2. Hali ya site jinsi ilivyokaa na udongo (Topography)
3.Upatikanaji wa Mafundi na Vibarua
4. ubora wa fundi mwenyewe au uzoefu
na vingine vingi, hivi vinapelekea gharama kupishana kulingana na eneo husika mathalani nyumba ya vyumba 3 yenye ukubwa wa mita za mraba 120 haiwezi lingana na nyumba ya vyumba vitatu yenye ukubwa wa mita za mraba 150, Gharama ya kujenga kigamboni inaweza isifanane na gharama ya Mbezi beach, au Dodoma na Dar gharama hazifanani. Nachoweza kukushauri ni fanya utafiti kwa wenyeji wa Eneo lako ujue walitumia gharama kiasi gani au gharama za mafundi wa eneo husika, jaribu kulinganisha hata mafundi wa 3 utapata gharama ya kuanza mradi wako
 
Kwa nyumba ya vyumba vitatu kwa jinsi alivyo nidadafulia ,

Ukuta unakula tofali80 piga*4=320 tofali kwa kila chumba mara vyumba vitatu jumla tofali 960 bado sebule otherwise isiwe kama haina sebule ila kama inasebule maximamu tofali 1500 *500 ya fundi= jumlisha beam iyo out of tofali beam ina gharma zake.

Then atapandisha course mbili juu y beam matofali kama 200 nyumba nzima hapo msingi sijaweka so gharma za ujenzi wa msingi matofali 800 *500 + 1700*500+beam utapata jibu Ila kama

Nina fundi wangu kazi zake nazikubali mno mno na ktk kuelewana nae ni muelewa sio mtu wa kulalia kama utakua okey nikupe namba zake ntamdirect kwako for sure nahis nyumba itakamilika hadi kupaua kama utakua upo njema
 
Kwa nyumba ya vyumba vitatu kwa jinsi alivyo nidadafulia...
Nakushukuru mkuu KWA msaada wa mawazo.Nadhani kuna aina ya upigaji maana ameniambia tofari za msingi tu ni 1255
Ila alisema ameweka kujenga tofari moja 500 KWA sababu amekadiria ili gharama za msingi na zege la lintazipo ndani ya pesa hiyo
 
Nawasalimu wanajamvi wote,hongereni KWA majukumu ya kujenga taifa. Leo nimekuja kwenu kuomba ushauri ni kipino gani kinatumika kupata bei ya ujenzi wa nyumba?
Nimempata fundi aniinulie boma kuanzia msingi hadi kwenye hatua ya lenta,mahesabu yake aliyopiga ni shs 500 KWA tofari moja gharama itahusu pia kuchimba msimgi na gharama ya kumwaga zege la beam.
Je wewe ulitumia njia gani kupataa gharama ya ujenzi? Nitashukuru sana lwa mchango wenu wa mawazo.
Baada ya kupiga mahesabu jumla imefika milioni laki saba

Mkuu ushauri wangu tafuta mafundi kama watano karibu na site wapeleke hapo kila mmoja na wakati wake,utapata uhalisia wa bei. Kuna ghorofa nilishaikuta sehemu hadi inatia huruma. Kumbe tajiri kaleta mafundi mkoa mwingine,hawajui udongo wa yale maeneo,full kulipua
 
Back
Top Bottom