Msaada kuhusu gharama za fundi kujenga nyumba ya vyumba vitatu kuanzia msingi hadi kwenye beam

Msaada kuhusu gharama za fundi kujenga nyumba ya vyumba vitatu kuanzia msingi hadi kwenye beam

Nawasalimu wanajamvi wote,hongereni kwa majukumu ya kujenga taifa. Leo nimekuja kwenu kuomba ushauri ni kipino gani kinatumika kupata bei ya ujenzi wa nyumba?

Nimempata fundi aniinulie boma kuanzia msingi hadi kwenye hatua ya lenta,mahesabu yake aliyopiga ni shs 500 KWA tofari moja gharama itahusu pia kuchimba msimgi na gharama ya kumwaga zege la beam.

Je, wewe ulitumia njia gani kupataa gharama ya ujenzi? Nitashukuru sana lwa mchango wenu wa mawazo.

Baada ya kupiga mahesabu jumla imefika milioni laki saba

UVIMO ni jumuia ya mafundi ujenzi.
Shughuli zetu kuu ni ujenzi na umaliziaji nyumba.

Huduma zetu ziko katika fungate la

1-Ujenzi
2-Kupaua
3-Uselemara
4-Umeme
5-Magril na alminium
6-Kuchora na kusoma ramani..

Husuma zingine Ni
1-Kufanya fininishing za majengo aina yote
2-Kuchimba na kujenga mashimo ya maji na vyoo.

UVIMO tunapatikana Morogoro na Dar es salaam.

Tunafanya kazi nchi nzima :-
1-Tanzania bara
2-Tanzania visiwani (Pemba na Unguja)

UVIMO tukipata kazi kwa mteja wetu , kazi hukamilika kwa muda mfupi


Mawasiliano yetu ni
0753 961 896
0629 361 896
0753 927 572- Wasap
 
Ndugu karibu kuhesabu hiyo misingi iko mingapi ulafu uliza msingi utaenda chini kiasi kipi. Hapo utaelewa hiyo 150 ilio ongezeka itachimba msingi? Jihadhari naona hasara haiko mbali na wewe.
 
Ndugu jaribu kuhesabu hiyo misingi iko mingapi ulafu uliza msingi utaenda chini kiasi kipi. Hapo utaelewa hiyo 150 ilio ongezeka itachimba msingi? Jihadhari naona hasara haiko mbali na wewe.
 
Kama hiyo 500 kwa tofali moja ni pamoja na kuchimba msingi na umwagaji zege mpe iko sawa
 
Imagine Kuchimba, kujenga tofali, kukunja nondo, kutengeneza Formwork, kumwaga Zege mtu analipwa Chini ya Milioni 1 dah, life ni gumu sio poa
Ni kweli mkuu inasikitisha ila maisha ni magumu kuliko kuwa iddle bora hata upate kidogo japo kwa jasho jingi.

Natarajia kujenga nyumba ya vyumba 3 yenye square miter 95 kwa sh.800,000 tuu.
 
Nyumba zinazojengwa Kiubahili hivi huwa hazidumu na ama huja Kuungua na Moto au Kusombwa na Mafuriko ya Mvua za Masika kama si zile za Kushtukizwa na TMA.
Nawashahngaawengine bado wanamshauri ashushe bei
 
Gharama zinategemea vitu vingi sana, kwa uchache
1.Ukubwa wa Jengo
2. Hali ya site jinsi ilivyokaa na udongo (Topography)
3.Upatikanaji wa Mafundi na Vibarua
4. ubora wa fundi mwenyewe au uzoefu
na vingine vingi, hivi vinapelekea gharama kupishana kulingana na eneo husika mathalani nyumba ya vyumba 3 yenye ukubwa wa mita za mraba 120 haiwezi lingana na nyumba ya vyumba vitatu yenye ukubwa wa mita za mraba 150, Gharama ya kujenga kigamboni inaweza isifanane na gharama ya Mbezi beach, au Dodoma na Dar gharama hazifanani. Nachoweza kukushauri ni fanya utafiti kwa wenyeji wa Eneo lako ujue walitumia gharama kiasi gani au gharama za mafundi wa eneo husika, jaribu kulinganisha hata mafundi wa 3 utapata gharama ya kuanza mradi wako
Wewe utakuwa mjenzi
 
Nakushukuru mkuu KWA msaada wa mawazo.Nadhani kuna aina ya upigaji maana ameniambia tofari za msingi tu ni 1255
Ila alisema ameweka kujenga tofari moja 500 KWA sababu amekadiria ili gharama za msingi na zege la lintazipo ndani ya pesa hiyo
Bei rahisi mno mkuuu
 
UVIMO ni jumuia ya mafundi ujenzi.
Shughuli zetu kuu ni ujenzi na umaliziaji nyumba.

Huduma zetu ziko katika fungate la

1-Ujenzi
2-Kupaua
3-Uselemara
4-Umeme
5-Magril na alminium
6-Kuchora na kusoma ramani..

Husuma zingine Ni
1-Kufanya fininishing za majengo aina yote
2-Kuchimba na kujenga mashimo ya maji na vyoo.

UVIMO tunapatikana Morogoro na Dar es salaam.

Tunafanya kazi nchi nzima :-
1-Tanzania bara
2-Tanzania visiwani (Pemba na Unguja)

UVIMO tukipata kazi kwa mteja wetu , kazi hukamilika kwa muda mfupi


Mawasiliano yetu ni
0753 961 896
0629 361 896
0753 927 572- Wasap
Sawa
 
Back
Top Bottom