Kama chuo chako cha mwaka jana kilirudisha mkopo uliopewa, basi jiandae na kupata mkopo mwaka huu. Kama walitumia mkopo wako, jiandae kukalia jiwe.
Mwaka 2012 nilikua bodi ya mikopo kufuatilia mkopo wa mdogo wangu aliyeahirisha mwaka (2011). Cha ajabu nilikuta wanafunzi wengi wenye tatizo kama la mdogo wangu. Wengi wao walikua wamechaguliwa vyuo vya PRIVATE hapo awali na hawakuripoti, ila vyuo vyao vikatumia mkopo wao! Wale wanafunzi waliwajibika kulipa deni ili wapate mkopo upya.
Kuhusu kuwaona bodi ya mikopo, naona kwa sasa muda umeshaenda. Subiri matokeo kwanza. Yakitoka tofauti itabidi uwafuate! Huwa wanamajibu ya mkato, ila usikate tamaa kutokana na majibu yao!