Msaada kuhusu hili suala la mbwa kuua mwizi na mmiliki wa mbwa kufunguliwa shtaka la mauaji

Msaada kuhusu hili suala la mbwa kuua mwizi na mmiliki wa mbwa kufunguliwa shtaka la mauaji

Umeandika vema..... Kwa kuongeza...
Kumiliki mbwa ni Sawa na kumiliki silaha ya ulinzi... Hivo lazima ukasajiliwe kuwa una miliki silaha (mbwa) hapo utakuwa salama zaidi.
Ukimiliki mbwa unatakiwa ukasajiliwe wapi?
 
Tungeanza kwanza na posterm inasema nini juu ya chanzo cha kifo cha marehemu, pili kama marehemu sio sehemu ya ile familia, baada ya hapo sioni kosa la mwenye nyumba,
 
Msaada tafadhali juu ya scenario hii!

Kuna jamaa ana mji wake na katika mji huo ameweka ulinzi wa Mbwa hawa America Broiler pamoja na fensi, usiku kuna jamaa alienda kwa lengo la kuiba kwake alipofika eneo la tukio akaruka ukuta ili aweze kuingia ndani baada ya yeye kutua ndani akakutana na fujo za wale mbwa wakamng'ata mpaka jamaa akafa.

Mwenye nyumba kesho yake akaenda kutoa taarifa Polisi alipofika tu kutoa taarifa akakamatwa na kuwekwa kizuizini na kisha kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Je, hii iko vipi upande wa utetezi wa jamaa? Au jambo hili limekaa vipi kisheria?
Tatizo sheria zetu ni zakikoloni sana zinahitaji marekebisho makubwa..

Kuwekwa ndani ni kwa ajili ya kupata taarifa na kufanya uchunguzi

Mnachotakiwa ni kumtafuta mwanasheria na kumuombea dhamana wakati polisi wakiendelea na upelelezi wao..

Ila msiwe na shaka hatakuwa na shitaka la kujibu endapo atakuwa ameweka sign za kueleza kuna mbwa.
 
Msaada tafadhali juu ya scenario hii!

Kuna jamaa ana mji wake na katika mji huo ameweka ulinzi wa Mbwa hawa America Broiler pamoja na fensi, usiku kuna jamaa alienda kwa lengo la kuiba kwake alipofika eneo la tukio akaruka ukuta ili aweze kuingia ndani baada ya yeye kutua ndani akakutana na fujo za wale mbwa wakamng'ata mpaka jamaa akafa.

Mwenye nyumba kesho yake akaenda kutoa taarifa Polisi alipofika tu kutoa taarifa akakamatwa na kuwekwa kizuizini na kisha kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Je, hii iko vipi upande wa utetezi wa jamaa? Au jambo hili limekaa vipi kisheria?
Fursa ya rushwa!
 
Hili namba 2 kama linashinda gym vile [emoji16]
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Sikia ndugu io kesi lazima ifanyiwe uchunguz kwanza umejuaje km ni mwiz pili nn kilimuuq maana mbwa pekee yke not easy binadamu ana uwezo wa kuua mbwa ni minutes km upo strong
Una uwezo wa kuua mbwa mmoja labda bila silaha. Umevamiwa na mbwa watatu American breeds wale kama Rotweiller, Pitbull ama hao Broiler kama alivyowataja mtoa mada.

These breeds are very aggressive and they do attack to kill kiasi kwamba ndani ya mda mchache wanaweza kukugeuza mboga.
 
Ukivamiwa na mbwa jitahid sana usidondoke,then pambana nae ukiwa umesimama hapo utawin
 
Ogopa maiti akikutwa katika eneo lako! Hata kama hukuua,lazima uisaidie polisi katika upelelezi.
 
Duh kwa hiyo hao mbwa walimsahau hadi mfanyakazi wa hapo,kama ni hvyo hawana masihara
Jamaa aliruka fence kumbuka na wao katika kufundishwa kwao ni kuwa hakuna kinachoingia chochote baada ya wao kufunguliwa. Sasa yule jomba akajua watamjua tu au watamkaushia kama ilivyo kwa walinzi wa shule wakikunyaka.
 
Hapo Mchawi CCTV tu!!

Kweli ni Muhimu kuweka Alert(Warning) kwamba KUNA MBWA WAKALI au HATARI ELECTRIC FENSE.
 
Io ndio polisi nimeuliza apo juu watu wakaniona mm mjinga lazima wakuulize una uhakika gan km ni mwiz na sio kusema tu ni mwiz kisa karuka ukuta

Ameruka ukuta anatafuta nini? Huyo ni kibaka nayestahili yaliyompata!!! Mwenye mbwa hana kesi ya kujibu kwani kibaka ametresspass.
Inawezekana kibaka alipata kipigo mahala na katika hali ya kujihami akaruka ukuta na kuingia kwenye uzio ambamo akakutana na hao mbwa; ikawa hana uwezo wa kujitetea kifo kikamfika!
 
Ni American Pitbull au American Broiler? Navyojua broiler ni aina ya kuku wa kisasa maalum kwaajili ya nyama (Wanakua kwa haraka na wakubwa).

Anyway, turudi kwenye mada husika.

Sheria inasema unapoweka ulinzi wa kutumia "WANYAMA WAKALI au UMEME" ni lazima uweke kibao kwa nje kwenye geti la kuingilia nyumbani au ukutani kinachotoa "TAHADHARI/ONYO (Warning Sign)" juu ya uwepo wa hivo vitu.

Mfano, TAHADHARI KUNA MBWA WAKALI" au "TAHADHARI KUNA FENCE YA UMEME".

Ukifanya hivo ukaweka tahadhari nje ya uzio wako, basi atakaeingia ndani kwako iwe mwizi au mtu unaemfahamu au jirani tu, akapata madhara, unakua hauhusiki kwa lolote litakalo mtokea. Anakua amekaidi tahadhari uliompa.

Ila usipofanya kuweka tahadhari, basi mtu yoyote akidhurika utawajibika kwa tatizo lolote litakalo tokea kutokana na hivo vitu vyako vya ulinzi.

NOTE: Nia na madhumuni ya kuwepo kwa sheria, ni kwaajili ya kulinda haki za watu (hata kama mtu ni mwizi au muuwaji ila kuna sheria zinazolinda utu wake).
Hili nalo la kuangalia. Haswa la mbwa; maana linaondoa ile hali ya surprise kwa mwizi. Ukiandika kuna mbwa, mwizi naye anajipanga namna ya kummaliza mbwa kabla ajafanya wizi wake.
 
Kesi ni ngumu pengine jamaa alikuwa anamdai huyo boss alafu akamwaidi njoo nyumbani achukue hela na kufungulia mbwa,
Sasa hilo si ataambiwa tu athibitishe kama alikuwa anamdai!! Hakuna kesi ngumu hapo.
 
kuuawa na mbwa nao ni uzembe.

yule kiumbe mbali na meno makali hakuzidi kwa chochote,labda kibaka alikuwa ni wale wanaotumia madawa ya kulevya.
 
Back
Top Bottom