Msaada Kuhusu Hizi Air Cooler

Msaada Kuhusu Hizi Air Cooler

Baba Rhobi

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2020
Posts
1,611
Reaction score
2,881
Wakuu wa Tech inakuaje....!?
Wakuu na amini tunatofautiana uwezo kimapato wapo wanaomudu gharama za kulipia AC nikiwa nacheki Youtube review za AC nakuta kwa 24Hrs ngoma imebeba Units kama 20 hivi hii ukizidisha na 300 ushee bei ya unit 1 mara 30 staki hata kujua jibu lake.

Kiukweli hizi fan hua hazipunguzi joto zinachofanya ni ku circurate ile ile hewa yenye joto.
Ndipo zinakuja hizi Air cooler vipi ambao mmewai kuzitumia vipi ufanyaji kazi wake ukoje...!?
Je ni kweli zenyewe walau zinapunguza joto make naona zenyewe zinatumia maji vipi mlo wai zitumia au nazo ni msala tu na Maskini tukimbilie wapi wakuu.
IMG_20241004_120501.jpg
 
Kwa ujumla ni hovyo hasa kwa hali ya hewa ya DSM, zinahitaji low humidity hewa ya moto kavu, kufanya chochote angalau 30%->50% kwenda chini DSM humidity ni 70-80%
 
Kwa ujumla ni hovyo hasa kwa hali ya hewa ya DSM, zinahitaji low humidity hewa ya moto kavu, kufanya chochote angalau 30%->50% kwenda chini DSM humidity ni 70-80%
Du! Hatari sana kumbe watu ni kupigwa tu za kichwa kwa kutokujua, sijui huku Mwanza Humidity ikoje.
 
Usichezee hela aisee. Humidity (kiwango cha maji kwenye hewa) kwa DSM ipo juu sana. Inafaa mikoa ya arid/semi-arid.

Kwa Dar labda zile kubwa sana. Otherwise itumie kama feni.
 
Nasikia hizo air cooler hamna kitu
Mfano alichoweka iko pale Mlimani City Little Mall vinauzwa 140,000 Tsh, vinaitwa Aborder

Aisee ni utopolo. Ukiweka ivo vidude vya blue unaviweka kwenye friji vinaganda barafu ndio unaviweka kwenye iyo mashine, mara mia uwekeze kwenye feni ya kishua.
 
Mfano alichoweka iko pale Mlimani City Little Mall vinauzwa 140,000 Tsh.

Aisee ni utopolo. Ukiweka ivo vidude vya blue unaviweka kwenye friji vinaganda barafu ndio unaviweka kwenye iyo mashine, mara mia uwekeze kwenye feni ya kishua.
Fan za kishua zikoje mkuu
 
Hizo zinatoa upepo wenye ubaridi
Hazina kelele
Zinachuja vumbi
Haziumizi kifua, anatumia mtoto au mtu mzima bila.shida

Ninazo za mtumba nyingi sana ninaziuza hapa Dar es salaam
karibu😁
Weka bei na mawasiliano. au hizi sifa ni kwa kuwa uzaziuza Mkuu? 😀
 
Back
Top Bottom