Nina ndugu yangu alikuwa ameolewa ndoa kanisani, waliishi miaka 12 ya ndoa.
Mume akaja kuanzisha maisha mapya na mwanamke mwingine, alikuwa ni mwanajeshi wanaishi katika nyumba za jeshi mke akaenda kwa ndugu zake mkoa huu hapa Arusha, mume akawa anaenda kulala kwa huyo mwanamke aliempangia chumba sehemu nyingine maana hakutaka kumpeleka kwenye nyumba aliyokuwa anakaa na mke.
Bahati mbaya siku moja anatoka kwa huyo mwakamke kwenda kwenda kazini akapata ajali akafariki dunia. kesi ya mirathi ikafunguliwa lakini yule hawara alikuwa ana ndugu yake alikuwa ni hakimu wa hiyo mahakama akampa ile cheki ya mirathi, mke wa marehemu akawa akienda mahakamani anaambiwa faili halionekani, hapo ni miaka miwili ya kufuatilia hiyo mirathi, karani akamuonea huruma na kumuambia ukweli cheki alishapewa mwenzake na hivyo hapo anazungushwa ili aache.
Akafungua kesi nyingine na yule mwanamke akatafutwa akashikwa akakubali kuchukua hela akasema akajengea nyumba ila atamlipa kwa kuwa eti na yeye alizaa na marehemu, ila akakubali kumlipa huyo mwenzake kiasi cha hela, akapewa dhamana na alie mdhamini ni mama yake mzazi. Sasa miaka inazidi kwenda mtuhumiwa haonekani na mama haji mahakamani ndugu yangu anahitaji msaada wa kumpatia haki yake kwani anaishi maisha magumu na watoto nayeye alikuwa mama wa nyumbani ila sasa anafanya biashara ndigondogo.
SAMAHANI KWA MAELEZO MAREFU. ASANTE KWA KUSOMA.