Msaada kuhusu matrekta ya Massey Ferguson

Msaada kuhusu matrekta ya Massey Ferguson

NusuMutu

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
421
Reaction score
87
Heshma mbele wadau,
Nimeamua kufanya kilimo sehemu za eastern na central zone,nilikuwa nahitaji trekta na kwasababu nguvu yangu kipesa si kubwa sana nimeona nitafute used tractor (napendelea Massey Ferguson) ila sijajua kwa hali yetu huku ni model gani itanifaa zaidi,ila kwa kuanzia nilikuwa nina wazo la model ya MF 3075-3090 ambayo ni Horse Power 75-99 sasa sijajua spareparts zake upatkanaji wake hapa, kama yana usumbufu wowote na fuel consumption.
Wadau wenye uelewa zaidi wa matrekta haya naomba tupeane elimu.
Nawasilisha.
 
ni model gani kati ya hayo yenye HP 75-99 itanifaa kwa hapa kwetu? ndio swali. Mkuu nimeshajaribu kuakses webs kadhaa za wauzaji nimejua specs na bei pia..

MF-185

P_154_C_1.jpg

SOURCE: belltractors.com
 
MF-185

P_154_C_1.jpg

SOURCE: belltractors.com

Mkuu unaweza kutoa maelezo kidogo ku-justfy ushauri wako? je wewe ulishawahi litumia trekta hilo kwa kilimo? kama ndio,vipuri? mafuta? hebu toa maelezo kidogo manake matrekta yanafanya kazi nyingi mengine hata hapo dar es salaam bandarini yapo yanavuta makontena
 
kwa ujumla MF ni matrekta mazuri maana sisi huwa tunatumia nyumbani.sina uhakika model ipi ni nzuri kwako il sisi tunazo mbili MF 88 na MF 65 ni mazuri na spare zake kupatikana ni rahisi sana na return yake ni ya muda mfupi. nikisema sisi namaanisha nyumbani kwetu. ila ni trekta nzuri kwa tanzania hasa maeneo ya Ifakara na morogoro kwa ujumla ndo na uzoefu nayo.
 
ukipata new model 240 massey ni nzuri sana inatumia mafuta kidogo wastani wa lita 30 kwa ekari 20, PIYA ANGALIA BEI YA TRECTA MASSEY USED SIO CHINI YA DOLA 12000= KWA RATE YA DOLA 1580*12000 = 18,960,000/= UKIENDA SUMA JKT UNAPATA TRECTA JIPYA FARM TRACT 60-70 KWA BEI YA 18,000,000/= BILA JEMBE UTUMIAJI WA MAFUTA NI MZURI SANA KWA HAYA MATRECTA YA SUMA JKT PIYA UNALIPA KWA AWAMU MWANZO UNALIPA MILIONI 9,000,000/= KIASI KILICHOBAKI UNALIPA KWA MIAKA MIWILI KWA USHAURI ZAIDI WA KILIMO NA JINSI YA KUPATA MASHAMBA CENTRAL ZONE NI PM SMS 0787 139327
 
Heshma mbele wadau,
Nimeamua kufanya kilimo sehemu za eastern na central zone,nilikuwa nahitaji trekta na kwasababu nguvu yangu kipesa si kubwa sana nimeona nitafute used tractor (napendelea Massey Ferguson) ila sijajua kwa hali yetu huku ni model gani itanifaa zaidi,ila kwa kuanzia nilikuwa nina wazo la model ya MF 3075-3090 ambayo ni Horse Power 75-99 sasa sijajua spareparts zake upatkanaji wake hapa, kama yana usumbufu wowote na fuel consumption.
Wadau wenye uelewa zaidi wa matrekta haya naomba tupeane elimu.
Nawasilisha.

NusuMutu kama alivyosema mdau mmoja hiyo MF horse power 75 linatosha sana kwa ardhi ya TZ, ukinunua zaidi ya horse powr hizo itakuwa kwako kwa upande wa mafuta, na ukinunua chini ya hapo kwenye udongo mgumu litachemsha. Bahati nzuri mimi ninalo, tena nataka kuliuza kwa sababu ya kukosa msimamizi (sasa hivi niko nje ya nchi). Ila ukifika bei nitakuuzia, nilinunua mpya mwaka 2008, na nimelitumia kwa miaka miwili tu nikapata safari ya ghafla nikaondoka, hivi sasa lipo tu linafanyakazi ndogo tu. Lina kila kitu, jembe, harrow, na tela la kubinua lenyewe (hydraulic treiler). Ukiwa-interested niPM
 
Horse power 75 linatosha sana mkuu kwa TZ inashauriwa tractor isiwe chini ya horse power 55,Kwa Suma JKT Farm Track ni vimeo bora ununue New Holland lakini MF ni nzuri kwa TZ cause spare parts zake zinapatikana kirahasi,kama unaweza kupata John Deere ni ya ukweli zaidi na spare parts zake zimeanza kupatikana nchini japo sio sana kama MF ila zina nguvu sana
 
Kuokoa wino mi ngoja nikuite 7yi! Hapo vp?(itikia , hapo powa!) asante kwa ushauri wako,naufanyia kazi.unajua nilipita pale suma jkt wakati mmoja lakini sikuridhika sana nafsi yangu.n way tuyaache hayo. pia nimeona matrekta ya John Deere kwa kweli ni ya ukweli lakini pia niya gharama kuanzia bei zake, spare parts zake ukiachilia mbali upatkanaji wa mafundi wake espeshali litakapokufia wakati upo shamba huko porini.thanks dude
 
Farm Trac ni kimeo mwisho ndo maana wanashindwa kuwapenei miaka 6 ya kulipia........ile ni mifano ya Matrekta;

MF ni nzuri lakini mie nina
MF 595 hP 90 na JD Hp 110 ...ni pm tuongee
 
Kuokoa wino mi ngoja nikuite 7yi! Hapo vp?(itikia , hapo powa!) asante kwa ushauri wako,naufanyia kazi.unajua nilipita pale suma jkt wakati mmoja lakini sikuridhika sana nafsi yangu.n way tuyaache hayo. pia nimeona matrekta ya John Deere kwa kweli ni ya ukweli lakini pia niya gharama kuanzia bei zake, spare parts zake ukiachilia mbali upatkanaji wa mafundi wake espeshali litakapokufia wakati upo shamba huko porini.thanks dude

Mkuu zile za JKT hasa Farm track ni vimeo usiguse labda New Holland,John Deere ni tractor za ukweli sana bei zake zisikutishe sana kuna site fulani nimeisahau kidogo ngoja niisake ntaiweka humu bei zake ni nzuri na kuhusu spare parts kuna wakala wao wapo Mikocheni pale wanakuja hadi site kukutengenezea hao jamaa nao pia wanauza John Deere lakini underlicense za India mpya kabisa na wanaweza kukusaidia kupata mkopo ila sikushauri sana ni bora ukachukua John deere ya ukweli Used ulaya naweza kukupa contacts pia za jamaa wenye John Deere wakakupa uzoefu na ni wapi wanapata spare parts.Still MF is a good brand for TZ ukikosa John Deere chukua MF cheap spare parts and cheap services.
Ukikuta kitu FIAT kipo kwenye hali nzuri usijiulize mara mbili pale Muitaliano alituliza akili ni za ukweli balaa ila hazipatikani kirahisi na spare parts hazipatikani.
 
Wakuu....kuna mtu yoyote amejaribi DONG FENG tractors toka china...mimi nalima shamba dogo hivyo natuma 20 HP ambayo ni 4WD na nzuri sana. Pia kwa anayehitaji WEEDING MACHINE anitafute, ni mfano wa power tiller lakini ni ndogo zaidi ambapo unapita nayo kwenye mistari ya mazao na kufanya palizi bila tatizo. Hii inanisaidia sana kwenye palizi ya nanasi baada ya kusumbuliwa sana na palizi ya jembe watu wanatumia wiki 2 kumaliza eka...sasa nimezipata na zinafanya kazi vizuri sana. Eka moja ni kama masaa matatu tu.
 
Wadau nawashukuruni sana.wote mmenipa mchango mzuri sana (na bado walio na uzoefu tunaweza kueleweshana zaidi) na sasa naanza kuifanyia kazi..
aksanteni
 
wadau nawashukuruni sana.wote mmenipa mchango mzuri sana (na bado walio na uzoefu tunaweza kueleweshana zaidi) na sasa naanza kuifanyia kazi..
Aksanteni

shime ndugu yangu kilimo ndilo jibu la msingi la ajira hapa kwetu mengine yote sanaa tuu
 
Hilo Trekta la MAssey Ferguson kama hilo kwenye picha ni kiasi gani?
 
Asante sana Mama Paroko . Msalimie 'Paroko'
 
Back
Top Bottom