Mimi ndio Kwanzaa nimeingia kwenye kilimo na nimelima hizo Assila F1 mpaka sasa zina siku 21 tangu nimehamisha shamban. .. Kwa nilichoona hawa cutworms walikula ila nilipiga Dudu All nikachanganya na Ridomill ajili ya ukungu, Baada ya siku 10 nikapiga tena Ridomill nikachanganya na Ebony M72, Baada ya siku tatu nikapiga Polyfeed Starter tare 5/6 nimeweka mbolea ya Yaramila. Kuna mdudu aliingia kwenye shina mbili nimepiga dawa ya Prove...Nyanya zinaendelea vizuri na sijawahi kunyeshea maji tangu nizipande shamban, Ila cutworms walinikaribisha shamban! Ningependa kujua kama kunao uwezekano wa kuwaua hawa minyoo kabla ya kupanda....?