mkuu nitahitaji msaada wako mimi ni mgeni wa mambo hayo na ni kama ki bustani hivi cha robo heka je mbegu nzuri ni ipi ? kulikuwa na mazao mengine hapo kama migomba n.k
1: Kama ndiyo unaanza kabisa Kilimo Cha Nyanya, Anza na Mbegu za Kawaida mfano: Rio Grande ni Nzuri,Tanya, Tengeru nk, ila Rio Grande ndiyo yenyewe
Nasema Anza na Mbegu hizi za Kawaida Kwa sababu Gharama za Matunzo siyo kubwa sana.Lakini pia Mavuno yake ni ya Wastani, unaweza chuma michumo mitano basi.
Bei zake pia ni rafiki, kuanzia 3000/- nakuendelea.
2: Hizo Mbegu za F1 ambazo zipo za aina Mbali Mbali, ni Mbegu za Kisasa.Huzaa sana lakini pia unavuna muda mrefu.
Mbegu hizi huhitaji Matunzo sana na madawa ya kutosha, ukishindwa Matunzo utasema kilimo Cha Nyanya hakifai.
Bei zake ni ghali sana, maana Mbegu ya chini kabisa gram 10 ni zaidi ya 15,000/-
3:Hivyo angalia vigezo nilivyokueleza hapo juu then fanya uamuzi, pia waweza mshirikisha AFISA kilimo aliyekaribu yako