Msaada kuhusu mbegu za nyanya

Msaada kuhusu mbegu za nyanya

Kwa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 1000 inaingia miche mingapi ya nyanya??

Kwa upandaji wa mstari mmoja ni miche 1400 kwa mistari miwili ni 2800. Ukinunua mbegu unaongeza asilimia 30 kwa ile ambayo haitoota au itakufa uwe na ya kurudishia
 
Kwa upandaji wa mstari mmoja ni miche 1400 kwa mistari miwili ni 2800. Ukinunua mbegu unaongeza asilimia 30 kwa ile ambayo haitoota au itakufa uwe na ya kurudishia
Asante mkuu..
Kwann idadi ya miche inapishana sana kati ya upandaji wa mstari mmoja na mistari miwili?? Na pia kwa eneo kama hilo unahitaji gram ngapi za mbegu?
 
Asante mkuu..
Kwann idadi ya miche inapishana sana kati ya upandaji wa mstari mmoja na mistari miwili?? Na pia kwa eneo kama hilo unahitaji gram ngapi za mbegu?

Dah hilo swali kweli jamaa yangu kwa mstari mmoja lazima miche iwe michache ukipanda mistari miwili inamaana inakua double. Sema sasa mbegu pia itakupa aina ya upandaji most ya hizi hybrid za nnje (open field) ni za kupanda mstari mmoja sababu mche unakupa kg 6 mpaka nane ila kwa zile za kienyeji zinapandwa mistari miwili sababu kila mche unakupa tu kg 2 mpaka 3.

Kwa gm,mbegu chotara ziko kwa idadi ya mbegu mambo ya gm yanaanza kusahaulika sasa.
Ila uzito unategemea na aina ya nyanya mfano imara gm 1 ni mbegu 350 kampuni wanazidisha kidogo wakati wa kupima iwe faida kwa mkulima ila right kipimo ni gm 1 ya nyanya ni mbegu 250 mpaka 300
 
Nashukuru sana mkuu kwa ufafanuzi..
 
Karibu sana
Habari Mkuu.. nimekutana na hii chqngamoto.. baadhi ya mashina ya nyanya.. dawa gani inaweza kudhibiti huu ugonjwa??
20180314_175507.jpg
 
Habari Mkuu.. nimekutana na hii chqngamoto.. baadhi ya mashina ya nyanya.. dawa gani inaweza kudhibiti huu ugonjwa??View attachment 714706

Hiyo sio tatizo la mdudu wala sio ugonjwa ila ni tatizo la lishe,ni ukosefu wa Calcium ambao husababishwa na
1. Kutokuwekwa kwa mbolea yenye calcium kama CAN
2. Ukame hivyo calcium ya ardhini haipandi kwenye matunda maana husafirishwa na maji

Inaitwa BLOSSOM END ROT
 
Asante mkuu..kuhusu maji namwagia yakutosha.. kwahyo nikiweka mbolea ya CAN nitakua nimetibu tatizo..?
 
Hii nyanya ni ain gani? Hauna afya mmea wake vipi mbolea unawekaje?
Naona kuna uzee wa jani, kuna ukosefu wa madini na kuna ukungu + kutu. Unaweza yatoa majani ya chini kabla ya tunda la kwanza
Bro nakutafuta, naomba namba yako, nimekucheck inbox. Please
 
Niliichogundua ubahiri unatucost sana kwenye kilimo.Hatutaki kununua Pembejeo ili zitupatie mazao bora,matokeo yake mche hauna mbolea,haupuliziwi dawa kwa wakati mpaka tuone dalili ya ugonjwa.
 
mkuu the-horticulturist,aasante sana kwa elimu hii ;npo iringa,nilitaka kuuliza mbegu ipi ya hybrid inayorefuka ni nzuri kwa ukanda huu,pia mbolea ya CAN inafaa kuwekwa wakati gan?,maana kuna mtaalamu alisema unaweza kuchanganya CAN na DAP wakati wa kupanda!,Pia vip kuhusu mbolea ya maji ya Polyfeed?,msaada tafadhar....,
 
Umewatetea mkuu...niambie ukweli hawakuniuzia mbegu....nilinunua miche

Wandugu kwema?jamani naombeni mniambie mbegu inayoitwa Anna f1 ni nzuri?na vipi uzaaji wake na ninaweza kuipanda kwenye open space?au naombeni ushauri wa mbegu inayozaa sana na kwa mda mrefu kwa zaidi ya miezi 5 na zaidi,ahsanteni.
 
mkuu nitahitaji msaada wako mimi ni mgeni wa mambo hayo na ni kama ki bustani hivi cha robo heka je mbegu nzuri ni ipi ? kulikuwa na mazao mengine hapo kama migomba n.k
1: Kama ndiyo unaanza kabisa Kilimo Cha Nyanya, Anza na Mbegu za Kawaida mfano: Rio Grande ni Nzuri,Tanya, Tengeru nk, ila Rio Grande ndiyo yenyewe
Nasema Anza na Mbegu hizi za Kawaida Kwa sababu Gharama za Matunzo siyo kubwa sana.Lakini pia Mavuno yake ni ya Wastani, unaweza chuma michumo mitano basi.
Bei zake pia ni rafiki, kuanzia 3000/- nakuendelea.
2: Hizo Mbegu za F1 ambazo zipo za aina Mbali Mbali, ni Mbegu za Kisasa.Huzaa sana lakini pia unavuna muda mrefu.
Mbegu hizi huhitaji Matunzo sana na madawa ya kutosha, ukishindwa Matunzo utasema kilimo Cha Nyanya hakifai.
Bei zake ni ghali sana, maana Mbegu ya chini kabisa gram 10 ni zaidi ya 15,000/-
3:Hivyo angalia vigezo nilivyokueleza hapo juu then fanya uamuzi, pia waweza mshirikisha AFISA kilimo aliyekaribu yako
 
Back
Top Bottom