Habari wana JF, Kwa Muda sasa huu ugonjwa unaniletea shida japo nimejaribu kutumia dawa mbali mbali za hospitali na za asili lakini bado kwa kiasi flani hali sio nzuri. Nataka kujua kama ipo dawa ambayo inaweza kutibu hili tatizo kwa asilimia 100, na Je, huu ugonjwa unatibika na kuisha kabisa au dawa nyingi zilizopo zinasaidia kutuliza tu mashambulizi na sio kutibu kabisa..?
[emoji256] *UFAHAMU UGONJWA WA PUMU* [emoji256]
sangidaherbal.blogspot.com
[emoji298]Pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu zinazojulikana kitaalamu kama bronchioles. Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya
kupitishia hewa (bronchioles tubes) hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito (mucus) na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa
nje na hivyo kupumua kwa shida sana.
[emoji298]Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu. Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hwa nje,
[emoji263]MAKUNDI YA PUMU[emoji263]
[emoji298]Pumu imegawanyika katika makundi mawili;
[emoji117]1⃣Pumu ya ghafla (Acute asthma): Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika kati ya shambulizi moja na jingine.
[emoji117]2⃣Pumu sugu (Chronic Asthma): Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu, njia za hewa huzidi kuwa nyembamba zaidi.
[emoji271]AINA ZA PUMU[emoji271]
Bila kujali mgonjwa yupo katika kundi gani, ugonjwa wa pumu unaweza kugawanywa katika aina kuu nne, ambazo ni:-
[emoji117]1⃣.Pumu inayobadilika (brittle asthma):Kulingana na tabia ya kujirudia rudia kwa matukio ya ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili, ambazo ni
Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika(type 1 brittle asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japo mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.Aina ya pili ya pumu inayobadilika (type2 brittle asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulio la ghafla (asthmatic attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu.
[emoji117]2⃣.Pumu hatari isiyobadilika (status asthmaticus): Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na matumizi ya dawa kadhaa, mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka, na anaweza kupoteza maisha.
[emoji117]3⃣.Pumu inayosababishwa na mazoezi (Exercise Induced Asthma): Hali hii husababishwa na ufanyaji wa kupitiliza wa mazoezi ya viungo. Kwa kawaida wakati wa kufanya mazoezi mtu hupumua kwa kutumia pua na kupitia mdomoni. Hata hivyo wakati mwingine hutokea hewa aivutayo huingia ndani ikiwa haijapozwa vya kutosha puani na hivyo kusababisha ongezeko la mtiririko wa damu katika mishipa inayosambaza damu katika mirija ya kupitisha hewa. Hali hii husababisha kuvimba
kwa kuta za mirija hiyo na muhusika kupata shambulio la pumu. Aina hii ya pumu yaweza kudhibitiwa na dawa. Inashauriwa sana kwa watu wenye matatizo kama haya kupasha moto misuli kwa mazoezi mepesi (warming up)kabla ya kuanza mazoezi mazito na ya muda mrefu.
[emoji117]4⃣.Pumu inayosababishwa na aina ya kazi afanyayo muhusika (Occupational Induced Asthma): Wakati fulani, mazingira ya kazi yanaweza kusababisha kutokea kwa pumu hata kwa baadhi ya wafanyakazi wasio na tatizo hili. Mara nyingi aina hii huweza kuwatokea watu wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza matairi, vigae, rangi, kemikali mbalimbali, mbolea, chuma, unga na mbao.
sangidaherbal.blogspot.com
[emoji261]MAMBO YANAYOSABABISHA PUMU[emoji261]
[emoji298]Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha kutokea kwa pumu. Mambo hayo ni pamoja na
Matatizo ya kinasaba:
[emoji117]Matatizo ya kinasaba yamehusishwa na kutokea kwa karibu asilimia 90 ya ugonjwa wa pumu hususani kipindi cha utoto.
[emoji117]Uvutaji wa sigara au tumbaku kipindi cha ujauzito pia unahusishwa na kusababisha pumu kwa mtoto atakayezaliwa.
[emoji117]Maendeleo ya kiuchumi: Ugonjwa wa pumu umeonekana sana kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi ikilinganishwa na nchi zenye maendeleo na hali duni ya kiuchumi.
[emoji117]Magonjwa ya mapafu kama bronchitisVyanzo vya mzio (allergens)kama vile vumbi, vinyesi vya wanyama na baadhi ya vyakula.
[emoji117]Uchafuzi wa mazingira kama moshi na baadhi ya harufu kali.
[emoji117]Baadhi ya kemikali kwenye maeneo ya kazi hasa kwenye viwanda kama vya rangi, chuma, sementi na vigae.
[emoji117]Baadhi ya wagonjwa wanaotumia dawa za kushusha shinikizo la damu zilizo katika jamii ya beta-blockers kama vilepropanolol wapo katika hatari ya kupata shambulio la ugonjwa wa pumu.
[emoji117]Magonjwa kwenye mfumo wa kupumua yasabishwayo na baadhi ya virusi na bakteria kama vile rhinovirus, Chlamydia pneumonia au Bordetella pertusis.
[emoji117]Matumizi ya mapema sana ya baadhi ya dawa hasa antibiotiki kwa watoto yanaweza kubadilisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na hivyo kumfanya mtoto kuwa katika hatari ya kupata pumu.
[emoji117]Ongezeko la msongo wa mawazo huweza kusababisha pumu na matatizo katika mfumo wa upumuaji
[emoji117]Upasuaji wakati wa kujifungua(caesarian section): Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kujifungua kwa njia ya upasuaji huongeza uwezekano wa kupata pumu kwa vile njia hiyo yaweza kuathiri mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya maradhi
[emoji271]DALILI ZA PUMU[emoji271]
Dalili za ugonjwa wa pumu ni pamoja na
[emoji298]Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida (shortness of breath)
[emoji298]Kutoa sauti kama mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)
[emoji298]Kukohoa sana (chronic cough) hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.
[emoji298]Kubana kwa kifua.Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa kama amechanganyikiwa.
Matibabu ya pumu huusishwa umri, aina na kundi la ugonjwa.
Ukihitaji dawa ya kupona ugonjwa wako basi unaweza kunitafuta muda wwte ukiwa tayari
sangidaherbal.blogspot.com
Kwa ushauri na dawa za magonjwa mbalimbali wasiliana nami
+255 655 821 550
Sulayman Sangida