Fomu zilivyotengenezwa ni lazima ujaze sababu ya safari yako kwenye mfumo. Aliyetengeneza mfumo alitakiwa kuweka options zaidi ya mwanafunzi, mfanyabiashara au mtumishi wa Serikali... Mfano mtanzania anawaza kwenda nje ya nchi kutalii pia.
Hapo kwenye sababu ya safari jaza Biashara, fomu ikishakamilika na kupokelewa bado kuna hatua ya mahojiano ya ana kwa ana, hapo ndipo unapothibitisha kuwa una uwezo wa kifedha si kumiliki passport tu bali unaweza kumudu gharama zote za safari kama itatokea.
Lakini, kuna sababu gani ya kumiliki passport kama huna mpango wa kusafiri? Kama mpango upo basi anza na nchi zinazotuzunguka ....itakuwa rahisi zaidi.
Kila lenye kheri kwako!.