Mkuu umeeleza vizuri sana, risks za kupiga tofali mwenyewe ni kubwa na unachosave ni kidogoOn a roughly but serious note:
Kwa hesabu ya tofali 45, kwa tofali 4800 utahitaji simenti mifuko takribani 110. Kwa bei ya 20,000/- kwa mfuko ni 2.2M.
Mchanga kila tripu ikupe tofali 200, utahitaji tripu 24... bei ya mfano ni 50,000/- kila hivyo itakula 1.2M.
Fundi wa kupiga tuseme utamlipa 150 hadi 200 kwa tofali, tuweke 800k.
Jumla kuu ni 2.2M+1.2M+800k = 4.2M.
Hapo bado maji, hatujui kama ni ya kulipia au niaje... na ishu ya kumwagilia hizo tofali sijui itakuwa kwako au kwa mpigaji!
Weka laki hapo ziada ihusishe huduma kama hizo.
Wakati huo, tofali zilizo tayari zinauzwa 1000 hadi 1200.... jumla 4.8M hadi 5.8M sijui kuhusu usafiri.
Piga hesabu utajua kiasi cha kuokoa hapo, na muda wako na usumbufu wa kusimamia na kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora.
Laki tano hadi milioni unaweza kuokoa.
Kumbuka mwaka huu sio wa kupata raha sana.
Tofautisha tofali ya kupigiwa kiwandani ambazo nyingi zinakuwa vibrated blocks na zinapigwa na mashine. Compaction ya zile mashine ni kubwa ndio sababu wanaweza kuongeza ratio ya mchanga na tofali likatoka na uimaraMkuu tofali 45 kwa mfuko 1 wa cement ni kawaida na matofali yanatoka imara
Ndio na huwa yanakuwa imara tu
Inategemea na aina ya mashine anayotumia kupitia tofali pamoja na aina ya cement atakayotumia, cement ya 42.5 akitumia na vibrator bado atapata tofali zuriTofali 45 kwa mfuko? Si mchanga mtupu tu huo jamani....
Tofali 19 kwa mfuko!!! Ndio dili.
Ndio maana nikasema kuwa kuna nyumba na kuna mabati juu ya matofaliKwani mnazouziwa ratio yao unajua wanafanyaje?mfuko unatoa hd tofali 60 sheikh
Ghorofa mbona ukienda 25 blocks kwa mfuko ngoma imara kabisa wala hupati tabuInategemea na aina ya mashine anayotumia kupitia tofali pamoja na aina ya cement atakayotumia , cement ya 42.5 , akitumia na vibrator bado atapata tofali zuri
Ratio ya tofali 19 kwa mfuko labda Kama anajenga ghorofa
Tofali za nchi 5. Nilipanga kutumia cement no 42.5 kumbe ipo ya no 45 pia?Sishauri 45 kwa mfuko, kwanza tofali zako ni za nchi ngapi unataka kupiga? kama ni nchi sita piga 30 kwa mfuko na kama ni nchi 5 piga 35 kwa mfuko si zaidi...
Changamoto ya kutumia machine ya vibrator site huwa ni nini?Tofautisha tofali ya kupigiwa kiwandani ambazo nyingi zinakuwa vibrated blocks na zinapigwa na mashine . Compaction ya zile mashine ni kubwa ndio sababu wanaweza kuongeza ratio ya mchanga na tofali likatoka na uimara
Hizi utakazopiga wewe zitakuwa za kawaida maana sifikirii Kama utatumia vibrator site . Kutoa tofali 45 kwa mashine ya bam bam , ni hatari nyingine
Watu mnabwabwaja tu ili muonekane wazee wa viwango, ni aidha mnaishi kwa shemeji hamjui kitu au lengo lenu ni kukatisha tamaa wenzenu!
Mfuko tofali 19!!!!
Mara tofali 25!!!
We unafikiri hiyo tofali ungeuziwa 1000-1200? Mpigaji angefanya biashara kichaa namna hiyo!
Tofali zote unazoona zinauzwa mtaani huko ni wastani wa zaidi ya 40, na kila siku unaona zinaondoka na maghorofa yanainuka... jipe muda kuwauliza wapigaji japo wanaweza wasikwambie ukweli.
Huu mjadala wa ujenzi upo juu ya uwezo wenu hivyo mlipaswa kuuamkia na kukaa kwa kutulia.
Mfuko wa simenti kwa tofali za ujenzi wa nyumba, 32.5R au 42.5R inatoa tofali 40-50 tena ni zenye ubora wa kiwango cha juu.
Na huyu ni mpigaji wa mikono, kwa mashine zinaweza kuzidi hapo na zikafaa tu.
Acheni ubishani na mizaha, hii ni moja ya sababu mnaogopa kujenga.
Asante mkuu, nimekupata vizuri sana.Sure ,ni kweli mfuko wa cement unatoa tofali hadi 50 na zinakuwa imara,cha msingi ni uchanganyaji mzuri na kuimwagilia vizuri hata wiki kama una maji ya kutosha!...
Utaweza kununua mashine ya mil 2 plus kwa ajili ya project ya tofali 5000 tu?Changamoto ya kutumia machine ya vibrator site huwa ni nini?
Vipi nikikodisha?Utaweza kununua mashine ya mil 2 plus , kwa ajili ya project ya tofali 5000 tu , ?
Hivi hii mashine inauzwaga bei ghali sana?Ita fundi, tafuta bei ya materials, bei ya mashine kununua au kukodi, vibao pia; take a pen and a paper Piga hesabu!
Mie sijui maswali mengine mnaulizaga mnakuwa na malengo gani!
75% ya wauza tofali za nchi 5 hutoa 44- 45 kwa mfuko waliobaki wanatoa 50.Tofali 45 kwa mfuko? Si mchanga mtupu tu huo jamani....
Tofali 19 kwa mfuko!!! Ndio dili.
Hivi hii mashine inauzwaga bei ghali sana?
Asante mkuuMashine za BAM BAM(za kupiga kwa mikono) hizi nzuri ni kutoka mkoani ,za Dar nyingi sio nzuri wanatumia chuma chenye thickness ndogo na zinauzwa around 200-300k labda uende kutengeneza kwa requirement zako! Zenye Thickness nzuri imara ni zaidi ya 350k.
Zile za umeme ,lazima ununue Kinu cha kuchanganyia cement na mashine ya kufyatulia tofali kwa pamoja ambapo cost yake zote ina range kati ya 4m - 5m.
Pili ukishanunua mashine(BAM BAM au UMEME) lazima utenegeneza vibao vya kulaza tofali ikitenegenezwa!! Kwa BAM BAMA minimum vibao vya mifuko 10 na kwa mshine aleast vibao vya mifuko 20.
Mkuu ndio mchezo wao lakini ndo matofali yanayonunuliwa siku zote na yanatumika kujenga nyumba na watu wanaishi mpaka wanazeeka humoKutoa tofali 45 kwa mfuko mmoja wa cement
Ni aina nyingine ya UTAPELI.
wale wanaofyatua tofali za kuuza ndo mchezo wao huo.
Ila Kama unataka kufyatua zako mwenyewe usifanye huo mchezo.
Asante mkuu
Ila naomba kuuliza tena hiyo ya mkono ikoje? Na inaweza vizuri tu kufyatua matofali 4800?
Naomba kapicha kama hutajali
Mkuu ndo mchezo wao lakini ndo matofali yanayonunuliwa siku zote na yanatumika kujenga nyumba na watu wanaishi mpaka wanazeeka humo