Msaada kujua gharama ya kufyatua tofali 4,800

Msaada kujua gharama ya kufyatua tofali 4,800

Sishauri 45 kwa mfuko, kwanza tofali zako ni za nchi ngapi unataka kupiga? Kama ni nchi sita piga 30 kwa mfuko na kama ni nchi 5 piga 35 kwa mfuko si zaidi.

Pia hakikisha unatumia mashine ya bam bam, hii ya kibao si nzuri kwa hiyo ratio, pia angalia mchanga usio na udongo, hakikisha tofali linamwagiliwa asubuhi na jioni kwa wiki moja.

Ni vema ukatumia cement no 45 tofauti ya bei huwa ni 500 tu.

Pia kwenye mfuko wa cement kuna maelekezo jinsi ya kupata ratio ya tofali.

Hakikisha unasimamia ratio na umwagiliaji hii ni muhimu sana sana

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
On a roughly but serious note:

Kwa hesabu ya tofali 45, kwa tofali 4800 utahitaji simenti mifuko takribani 110. Kwa bei ya 20,000/- kwa mfuko ni 2.2M.

Mchanga kila tripu ikupe tofali 200, utahitaji tripu 24... bei ya mfano ni 50,000/- kila hivyo itakula 1.2M.

Fundi wa kupiga tuseme utamlipa 150 hadi 200 kwa tofali, tuweke 800k.

Jumla kuu ni 2.2M+1.2M+800k = 4.2M.

Hapo bado maji, hatujui kama ni ya kulipia au niaje... na ishu ya kumwagilia hizo tofali sijui itakuwa kwako au kwa mpigaji!

Weka laki hapo ziada ihusishe huduma kama hizo.

Wakati huo, tofali zilizo tayari zinauzwa 1000 hadi 1200.... jumla 4.8M hadi 5.8M sijui kuhusu usafiri.

Piga hesabu utajua kiasi cha kuokoa hapo, na muda wako na usumbufu wa kusimamia na kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora.

Laki tano hadi milioni unaweza kuokoa.

Kumbuka mwaka huu sio wa kupata raha sana.
Mkuu umeeleza vizuri sana, risks za kupiga tofali mwenyewe ni kubwa na unachosave ni kidogo
 
Mkuu tofali 45 kwa mfuko 1 wa cement ni kawaida na matofali yanatoka imara

Ndio na huwa yanakuwa imara tu
Tofautisha tofali ya kupigiwa kiwandani ambazo nyingi zinakuwa vibrated blocks na zinapigwa na mashine. Compaction ya zile mashine ni kubwa ndio sababu wanaweza kuongeza ratio ya mchanga na tofali likatoka na uimara

Hizi utakazopiga wewe zitakuwa za kawaida maana sifikirii Kama utatumia vibrator site. Kutoa tofali 45 kwa mashine ya bam bam ni hatari nyingine
 
Tofali 45 kwa mfuko? Si mchanga mtupu tu huo jamani....
Tofali 19 kwa mfuko!!! Ndio dili.
Inategemea na aina ya mashine anayotumia kupitia tofali pamoja na aina ya cement atakayotumia, cement ya 42.5 akitumia na vibrator bado atapata tofali zuri

Ratio ya tofali 19 kwa mfuko labda Kama anajenga ghorofa
 
Inategemea na aina ya mashine anayotumia kupitia tofali pamoja na aina ya cement atakayotumia , cement ya 42.5 , akitumia na vibrator bado atapata tofali zuri

Ratio ya tofali 19 kwa mfuko labda Kama anajenga ghorofa
Ghorofa mbona ukienda 25 blocks kwa mfuko ngoma imara kabisa wala hupati tabu
 
Sishauri 45 kwa mfuko, kwanza tofali zako ni za nchi ngapi unataka kupiga? kama ni nchi sita piga 30 kwa mfuko na kama ni nchi 5 piga 35 kwa mfuko si zaidi...
Tofali za nchi 5. Nilipanga kutumia cement no 42.5 kumbe ipo ya no 45 pia?
 
Tofautisha tofali ya kupigiwa kiwandani ambazo nyingi zinakuwa vibrated blocks na zinapigwa na mashine . Compaction ya zile mashine ni kubwa ndio sababu wanaweza kuongeza ratio ya mchanga na tofali likatoka na uimara

Hizi utakazopiga wewe zitakuwa za kawaida maana sifikirii Kama utatumia vibrator site . Kutoa tofali 45 kwa mashine ya bam bam , ni hatari nyingine
Changamoto ya kutumia machine ya vibrator site huwa ni nini?
 
Watu mnabwabwaja tu ili muonekane wazee wa viwango, ni aidha mnaishi kwa shemeji hamjui kitu au lengo lenu ni kukatisha tamaa wenzenu!

Mfuko tofali 19!!!!

Mara tofali 25!!!

We unafikiri hiyo tofali ungeuziwa 1000-1200? Mpigaji angefanya biashara kichaa namna hiyo!

Tofali zote unazoona zinauzwa mtaani huko ni wastani wa zaidi ya 40, na kila siku unaona zinaondoka na maghorofa yanainuka... jipe muda kuwauliza wapigaji japo wanaweza wasikwambie ukweli.

Huu mjadala wa ujenzi upo juu ya uwezo wenu hivyo mlipaswa kuuamkia na kukaa kwa kutulia.


Mfuko wa simenti kwa tofali za ujenzi wa nyumba, 32.5R au 42.5R inatoa tofali 40-50 tena ni zenye ubora wa kiwango cha juu.

Na huyu ni mpigaji wa mikono, kwa mashine zinaweza kuzidi hapo na zikafaa tu.

Acheni ubishani na mizaha, hii ni moja ya sababu mnaogopa kujenga.

Sure, ni kweli mfuko wa cement unatoa tofali hadi 50 na zinakuwa imara, cha msingi ni uchanganyaji mzuri na kuimwagilia vizuri hata wiki kama una maji ya kutosha!

Kupata tofali 4800 inabidi anunue mifuko 107 ya cement kwa idadi ya 45 kwa kila mfuko.

Mende moja ya 14.5 - 16m3 inachapa mifuko 21 hadi 24 ,Tukiweka Average ya mifuko 22 kwa mende hivyo itakulazimu kununua Mende 5.....Sio kila mchanga unafaa kwa tofali....Mchanga unatakiwa uwe laini kama mpana inabidi waumix na udongo kama ule wa kifusi.

Kukodisha mashine ni elfu 5 kwa siku na gharama za ufundi ni elfu 5 kwa mfuko, mafundi wakiwa watatu wanaweza kupiga mifuko 10 kwa siku, kwahiyo kwa idadi ya mifuko 107 wataimaliza kwa siku 11.

Gharama:-

1. Cement 16,000 x 107 = 1,712,000/=
2. Mchanga Mende 5 = 200,000 x 5 = 1,000,000/=
3. Gharama za mashine = 11 x 5,000/= 55,000/=
4. Gharama za ufundi = 5,000/= x 107 = 535,000/=

Kwakuwa utamwagilia mwenyewe na maji unayo uliyochimba bwawa(ya mvua) basi hatutajumlisha gharama zake.

Grand Total = 3,302,000/= Hapo utaokoa Tsh 1,500,000/= kama utanunua kwa @ Tsh 1000 kwa kila tofali hadi Site.
 
Ita fundi, tafuta bei ya materials, bei ya mashine kununua au kukodi, vibao pia; take a pen and a paper Piga hesabu!

Mie sijui maswali mengine mnaulizaga mnakuwa na malengo gani!
Hivi hii mashine inauzwaga bei ghali sana?
 
Kutoa tofali 45 kwa mfuko mmoja wa cement
Ni aina nyingine ya UTAPELI.
Wale wanaofyatua tofali za kuuza ndio mchezo wao huo.
Ila Kama unataka kufyatua zako mwenyewe usifanye huo mchezo.
 
Hivi hii mashine inauzwaga bei ghali sana?

Mashine za BAM BAM(za kupiga kwa mikono) hizi nzuri ni kutoka mkoani, za Dar nyingi sio nzuri wanatumia chuma chenye thickness ndogo na zinauzwa around 200-300k labda uende kutengeneza kwa requirement zako! Zenye Thickness nzuri imara ni zaidi ya 350k.

Zile za umeme lazima ununue Kinu cha kuchanganyia cement na mashine ya kufyatulia tofali kwa pamoja ambapo cost yake zote ina range kati ya 4m - 5m.

Pili ukishanunua mashine(BAM BAM au UMEME) lazima utengeneza vibao vya kulaza tofali ikitenegenezwa!! Kwa BAM BAMA minimum vibao vya mifuko 10 na kwa mashine atleast vibao vya mifuko 20.
 
Mashine za BAM BAM(za kupiga kwa mikono) hizi nzuri ni kutoka mkoani ,za Dar nyingi sio nzuri wanatumia chuma chenye thickness ndogo na zinauzwa around 200-300k labda uende kutengeneza kwa requirement zako! Zenye Thickness nzuri imara ni zaidi ya 350k.

Zile za umeme ,lazima ununue Kinu cha kuchanganyia cement na mashine ya kufyatulia tofali kwa pamoja ambapo cost yake zote ina range kati ya 4m - 5m.

Pili ukishanunua mashine(BAM BAM au UMEME) lazima utenegeneza vibao vya kulaza tofali ikitenegenezwa!! Kwa BAM BAMA minimum vibao vya mifuko 10 na kwa mshine aleast vibao vya mifuko 20.
Asante mkuu

Ila naomba kuuliza tena hiyo ya mkono ikoje? Na inaweza vizuri tu kufyatua matofali 4800?

Naomba kapicha kama hutajali
 
Kutoa tofali 45 kwa mfuko mmoja wa cement
Ni aina nyingine ya UTAPELI.
wale wanaofyatua tofali za kuuza ndo mchezo wao huo.
Ila Kama unataka kufyatua zako mwenyewe usifanye huo mchezo.
Mkuu ndio mchezo wao lakini ndo matofali yanayonunuliwa siku zote na yanatumika kujenga nyumba na watu wanaishi mpaka wanazeeka humo
 
Asante mkuu

Ila naomba kuuliza tena hiyo ya mkono ikoje? Na inaweza vizuri tu kufyatua matofali 4800?

Naomba kapicha kama hutajali

Yes ya Mikono inafyatua Tofali 4800 kwa siku 11 kwa siku wanafyatua mifuko 10.(Tofali 450)

BAM BAM - YA MIKONO
BAMBAM.png


YA UMEME
UMEME.png
 
Back
Top Bottom