Msaada kujua gharama ya kufyatua tofali 4,800

Msaada kujua gharama ya kufyatua tofali 4,800

Achana na standards za kiwanda wewe, that’s way too perfect... eti water should be clean, sand should be dry!!

Uliona wapi?

Hapa tunaongea uhalisia huku saiti na sio kwenye makaratasi.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
On a roughly but serious note:

Kwa hesabu ya tofali 45, kwa tofali 4800 utahitaji simenti mifuko takribani 110. Kwa bei ya 20,000/- kwa mfuko ni 2.2M.

Mchanga kila tripu ikupe tofali 200, utahitaji tripu 24... bei ya mfano ni 50,000/- kila hivyo itakula 1.2M.

Fundi wa kupiga tuseme utamlipa 150 hadi 200 kwa tofali, tuweke 800k.

Jumla kuu ni 2.2M+1.2M+800k = 4.2M.

Hapo bado maji, hatujui kama ni ya kulipia au niaje... na ishu ya kumwagilia hizo tofali sijui itakuwa kwako au kwa mpigaji!

Weka laki hapo ziada ihusishe huduma kama hizo.

Wakati huo, tofali zilizo tayari zinauzwa 1000 hadi 1200.... jumla 4.8M hadi 5.8M sijui kuhusu usafiri.

Piga hesabu utajua kiasi cha kuokoa hapo, na muda wako na usumbufu wa kusimamia na kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora.

Laki tano hadi milioni unaweza kuokoa.

Kumbuka mwaka huu sio wa kupata raha sana.
Hiyo cement 20,000 wapi hiyo?
 
Ita fundi, tafuta bei ya materials, bei ya mashine kununua au kukodi, vibao pia; take a pen and a paper Piga hesabu!

Mie sijui maswali mengine mnaulizaga mnakuwa na malengo gani!
We jiulize swali jepesi tu...anaeuza tofali faida anaipataje? Hiyo faida ndo inaokolewa hapa
 
Utaokoa takribani milioni mbili, kulinganisha na kununua zilizo tayari.
Kimahesabu ni sawa ataokoa pesa ila itabidi apoteze na muda kwa ajili ya usimamizi wakati tofali linafyatuliwa na umwagiliaji Maji wa tofali hizo, akishindwa hapo ni sawa na bure.
Utakuja kupigiwa tofali 60 kwa mfuko na zisimwagiliwe kiuhakika mafundi wakaishi kwa kuuza cement na pesa ya Maji .
 
Back
Top Bottom