On a roughly but serious note:
Kwa hesabu ya tofali 45, kwa tofali 4800 utahitaji simenti mifuko takribani 110. Kwa bei ya 20,000/- kwa mfuko ni 2.2M.
Mchanga kila tripu ikupe tofali 200, utahitaji tripu 24... bei ya mfano ni 50,000/- kila hivyo itakula 1.2M.
Fundi wa kupiga tuseme utamlipa 150 hadi 200 kwa tofali, tuweke 800k.
Jumla kuu ni 2.2M+1.2M+800k = 4.2M.
Hapo bado maji, hatujui kama ni ya kulipia au niaje... na ishu ya kumwagilia hizo tofali sijui itakuwa kwako au kwa mpigaji!
Weka laki hapo ziada ihusishe huduma kama hizo.
Wakati huo, tofali zilizo tayari zinauzwa 1000 hadi 1200.... jumla 4.8M hadi 5.8M sijui kuhusu usafiri.
Piga hesabu utajua kiasi cha kuokoa hapo, na muda wako na usumbufu wa kusimamia na kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora.
Laki tano hadi milioni unaweza kuokoa.
Kumbuka mwaka huu sio wa kupata raha sana.