MSAADA: Kupata muwasho, vijipele hatimaye maumivu makali kwenye kuta za uke mpaka kwenye kinena

pm umefunga.
Tumia vitamin B Complex, 3×2 kwa siku za awali, baada ya wiki anza kupiga 1×1 kila siku. unaweza ukatumia dawa hii kwa wiki 2 mfululizo au zaidi.
nakuhakikishia; siku ya 3-5 utakuwa umepata nafuu kubwa. ahsante
 
pm umefunga.
Tumia vitamin B Complex, 3×2 kwa siku za awali, baada ya wiki anza kupiga 1×1 kila siku. unaweza ukatumia dawa hii kwa wiki 2 mfululizo au zaidi.
nakuhakikishia; siku ya 3-5 utakuwa umepata nafuu kubwa. ahsante
Ngoja niifungue mkuu.
Samahani....
 

Pole sana.

Cha kwanza kabisa ni vyema ukafika kituo cha afya kilichopo karibu yako ili uonane na daktari.

Huenda ukawa ni mzio (contact allergic dermatitis) kulingana na maelezo yako. Ni vyema ukafanya uchunguzi kama ulibadilisha au ulivaa nguo mpya za ndani, kama kuna dawa/mafuta au kemikali yoyote ulitumia kabla ya muwasho kuanza.

Pia inaweza kuwa maambukizi ya maradhi ya ngozi ambayo huambukizwa kwa njia ya kugusana mfano HSV ambayo husababisha vipele na kuwashwa.

Kwa hiyo nenda hospitalini ukaonane na daktari ili akufanyie uchunguzi ili upatiwe matibabu sahihi.

Kila la kheri.
 
Asante sana Dr PL , sawa nimekuelewa Daktari.
Na nilikuwa huko tangu asubuhi na wameniambia tatizo ni allergy ya bidhaa za mpira za Latex....na wamenipa na dawa.

Huwa natumia sana condom za ZANA, sasa zina ile mafuta yake nadhani ndio iliniletea hali hii ya maambukizi.
Asante sana kwa ushauri wako mpendwa.
 

Tahadhari:

-pamoja na ushauri unaotolewa hapa kuwa makini sana na epuka kutumia dawa zozote unazoshauriwa hapa. Ni vyema daktari akufanyie uchunguzi ili upatiwe dawa sahihi. Unaweza kuambiwa tumia dawa fulani ambayo pengine si sahihi kwa tatizo lako.

Kila la kheri.
 
Asante kwa ushauri Dr PL
Juzi nilienda hospitali na ikagundulika ni allergy ya bidhaa za mpira za latex, nimeshapatiwa matibabu.
Shukrani sana kwa ushauri na naendelea vyema tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…