SuperImpressor
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 1,505
- 648
Lilimegwa kimakosa, yaani aliyewaonyesha naye aliwaonyesha kimakosa naye alianza pia kujilaumu.Limemegwa kwasababu ipi? kuacha nafasi kwaajili ya kupitisha miundombinu kama barabara, umeme, maji, mitaro? Kama sababu ni hizi huna cha kudai kwenye upimaji shirikishi
Hatari iko kwenye kugharamia, noma kweli.Barabara rasmi ni hiyo iliyopimwa na si hiyo unayoisema wewe. Upimaji ulifanyika lini na wewe umegundua tatizo lini? Huwa kuna muda wa mapingamizi kabla ya hati kutoka. Kama hati hazijatoka unaweza kurudi kwa uongozi wa mtaa kuwaomba muende ardhi kuomba mkabadili mchoro, hapa itabidi uwaambie upo tayari kugharamia gharama zote za wajumbe, majirani na wapimaji watakapokuja tena kwasababu itaathiri maeneo ya wengine pia
Kosa lilifanyika wakati wa kuhakiki viwanja maana mwenye uwanja hakuhusishwa.Kwenye kuweka biconi hawamuulizagi mtu mipaka ya kiwaja chake,huwa wanauliza mipaka pindi wakiwa wanahakiki viwanja,baada ya hapo wanakujaga na vipimo vyao tayari ni mwendo wa kuweka biconi tu kulingana na vipimo vya kwenye ramani yao
Mimi mwenyewe yalinikuta hayo kule eneo la Boko, jirani yangu alimega sehemu lakini niliporipoti ramani haikubadilishwa.Nimesubiria sana nipate majibu jamani, kwani hakuna mtu aliyewahi kupatwa na hilo ama kulisikia kwa jirani?
Sent from my cupboard using mug
LoMimi mwenyewe yalinikuta hayo kule eneo la Boko, jirani yangu alimega sehemu lakini niliporipoti ramani haikubadilishwa.
Mimi wakati wa kuhakiki viwanja nilikuwepo na kiwanja changu kilihakikiwa vizuri ,wamekuja kuweka bikoni upande mmoja wakachukua hatua kadhaa kwa ajili ya barabara upande mwingine wakamega eneo kubwa kweli bicon yao wakaingiza ndani ya kiwanja changu sehemu kubwa tu,Nimeamua kuachana naoKosa lilifanyika wakati wa kuhakiki viwanja maana mwenye uwanja hakuhusishwa.
Sent from my cupboard using mug
Kwa hiyo ni kama kamchezo fulani walicheza, maana hapo walifanya kinyume na vipimo vya mwanzo.Mimi wakati wa kuhakiki viwanja nilikuwepo na kiwanja changu kilihakikiwa vizuri ,wamekuja kuweka bikoni upande mmoja wakachukua hatua kadhaa kwa ajili ya barabara upande mwingine wakamega eneo kubwa kweli bicon yao wakaingiza ndani ya kiwanja changu sehemu kubwa tu,Nimeamua kuachana nao