Msaada Kurekebisha Alama za Beacon Kwenye Uwanja

Msaada Kurekebisha Alama za Beacon Kwenye Uwanja

SuperImpressor

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
1,505
Reaction score
648
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu,

wapimaji wa viwanja walipita mahali fulani wakafanya upimaji kwa kuelekezwa na mtu mwingine kuhusu mipaka ya uwanja ilivyokaa,

lakini walielekezwa kimakosa bila mmiliki wa uwanja kuwepo, na mmiliki alipofika huko kakuta ardhi yake imedokolewa, sasa naomba kujua kuwa je kuna uwezekano kufanya marekebisho kwa kurudia kupima?

Maana jamaa alipofuatilia kwa uongozi wa mtaa ambao ndio waliokuwa wanawapitisha wapimaji kwenye viwanja, akaambiwa hapo itakuwa ngumu maana vipimo vimeshaingizwa kwenye mfumo.

Naomba kujua hilo maana asijepoteza haki yake.

Sent from my cupboard using mug
 
Nimesubiria sana nipate majibu jamani, kwani hakuna mtu aliyewahi kupatwa na hilo ama kulisikia kwa jirani?

Sent from my cupboard using mug
 
Limemegwa kwasababu ipi? kuacha nafasi kwaajili ya kupitisha miundombinu kama barabara, umeme, maji, mitaro? Kama sababu ni hizi huna cha kudai kwenye upimaji shirikishi
 
Limemegwa kwasababu ipi? kuacha nafasi kwaajili ya kupitisha miundombinu kama barabara, umeme, maji, mitaro? Kama sababu ni hizi huna cha kudai kwenye upimaji shirikishi
Lilimegwa kimakosa, yaani aliyewaonyesha naye aliwaonyesha kimakosa naye alianza pia kujilaumu.

Na kumegwa huko ni kwa upande wa kuweka njia. Na njia ilikuwepo tayari lakini katika njia hiyo kulikuwa na mti uliohitajika kukatwa ili kama ni gari lipite kirahisi.

Sasa kwa sababu mti ulikuwepo magari yakajitengenezea njia nyingine ambayo si halali, hivyo wapima viwanja walipopita wakaonyeshwa hiyo njia ya muda badala ya ile njia rasmi. Na hiyo ni kwa sababu mwenye uwanja hakuwepo.

Swali langu hasa ni kutaka kujua kama kuna uwezekano wa kufanya marekebisho endapo wale jamaa wataridhia baada ya kuelekezwa kwa usahihi.

Sent from my cupboard using mug
 
Barabara rasmi ni hiyo iliyopimwa na si hiyo unayoisema wewe. Upimaji ulifanyika lini na wewe umegundua tatizo lini? Huwa kuna muda wa mapingamizi kabla ya hati kutoka. Kama hati hazijatoka unaweza kurudi kwa uongozi wa mtaa kuwaomba muende ardhi kuomba mkabadili mchoro, hapa itabidi uwaambie upo tayari kugharamia gharama zote za wajumbe, majirani na wapimaji watakapokuja tena kwasababu itaathiri maeneo ya wengine pia
 
Hatari iko kwenye kugharamia, noma kweli.

Apambane atakavyoweza aisee.

Sent from my cupboard using mug
 
Kwenye kuweka biconi hawamuulizagi mtu mipaka ya kiwaja chake,huwa wanauliza mipaka pindi wakiwa wanahakiki viwanja,baada ya hapo wanakujaga na vipimo vyao tayari ni mwendo wa kuweka biconi tu kulingana na vipimo vya kwenye ramani yao
 
Kosa lilifanyika wakati wa kuhakiki viwanja maana mwenye uwanja hakuhusishwa.

Sent from my cupboard using mug
 
Nimesubiria sana nipate majibu jamani, kwani hakuna mtu aliyewahi kupatwa na hilo ama kulisikia kwa jirani?

Sent from my cupboard using mug
Mimi mwenyewe yalinikuta hayo kule eneo la Boko, jirani yangu alimega sehemu lakini niliporipoti ramani haikubadilishwa.
 
Kosa lilifanyika wakati wa kuhakiki viwanja maana mwenye uwanja hakuhusishwa.

Sent from my cupboard using mug
Mimi wakati wa kuhakiki viwanja nilikuwepo na kiwanja changu kilihakikiwa vizuri ,wamekuja kuweka bikoni upande mmoja wakachukua hatua kadhaa kwa ajili ya barabara upande mwingine wakamega eneo kubwa kweli bicon yao wakaingiza ndani ya kiwanja changu sehemu kubwa tu,Nimeamua kuachana nao
 
Kwa hiyo ni kama kamchezo fulani walicheza, maana hapo walifanya kinyume na vipimo vya mwanzo.

Sent from my cupboard using mug
 
Back
Top Bottom