Msaada, kuumwa kichwa (tatizo sugu)

Ilikua inachuja mwanga ndio, na ilinisaidia nimekaa miaka kadhaa sijaumwa ila kimerudi kwa kasi
hata siangalii vitu vyenye mwanga mkali wala mwanga hafifu, ni ubao na madaftari
 
Wingi wa damu pia huchangia. Angalia mazingira yako ya kazi huenda yakawa sababu.
Hili lilishawahi nitokea wakati nikiwa kijana, lilinitesa kwa muda mrefu, mwisho ikagundulika nilikuwa na damu nyingi, lakini shiada haikuwa tu damu nyingi, pia ilikuwa nzito, nilijitahidi kunywa maji kwa wingi tatizo likaisha, mpaka leo hii nikipunguza maji naumwa na kichwa sana. Pia maji yananisaidia ku balance weight.
 
Damu iko kawaida
Angalia marashi unayotumia mfano pafyumu, sprey ya ndani au kwenye gari, fen ofisin au nyumbani, kama unafanya ktk kiwanda cha kutengeneza sumu au usindikaji wa vitu vyovyote vyenye harufu kali, mwanga mkali ktk cm au computer
 
Kuumwa kichwa kinasababishwa na mambo mengi mno,kuna watu wameenda hospitali na hospital,wengine pia hupona tu ghafla kama kinavyooanza,fanya research,maumivu yakizidi muone daktari,pengine ni chemical imbalance mwilini zikikaa sawa kinapona chenyewe,kunywa maji

edit-hormone imbalance maybe due to menopause
 
Mmmh menopause kwenye 20,s
 
Unaniogopesha
Nenda pale Upanga Eye Center wana vipimo vyote vya macho including hiyo pressure ya macho.Kama una imani ya kutosha pia ningekushauri ukaombewe yawezekana una mapepo,hutapungukiwa kitu kwani nimesha shuhudia watu kadhaa wakiwa na hiyo shida na walipoombewa ikadhihirika ni yenyewe.
 
Ushaur wa kitaalm
Maumivu ya kichwa yanawezakua na sababu mbalimbali..inategemea na kichwa kinauma vp, but kutokana na maelezo yako inaonekana utakua na MIGRAINE, **** hujawahi tumia dawa inayoitwa ERGOTAMINE(VASOGRINE), hua ni nzur sana kwa migraine..jaribu kununua hio
 
Ahsante kuna doctor mwingine pia kanambia hicho kitu migraine headache, nitaenda kupima.... Nashukuru
 
Ahsante bestie, ila mapepo sina nshaombewa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…