Msaada: Kwa anayefahamu shule nzuri maeneo ya viwege

Hot27

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2020
Posts
372
Reaction score
691
Habari za wakati huu wakuu. Mwezi wa 8 tunategemea kuhamia kwenye makazi mapya maeneo ya Viwege msikitini. Nina wadogozangu wawili ambao mmoja yupo shule ya msingi na mwingine kidato cha tatu maeneo ya Mwananyamala. Kutokana na hali ilivyo tunatazamia kuweza kuwahamisha iliwawe karibu na nyumbani hivyo naomba kuuliza kwa wenyeji wa Viwege au wenye ufahamu wa maeneo hayo au ya jirani na hapo ni shule gani nzuri naweza wahamisha wadogozangu. Nikisema shule nzuri namaanisha mazingira na taaluma pia ila taaluma inaweza kuwa ya kwanza.
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
 
Private au serikali!?ufaulu wao ukoje!?
Kwa primary kama ni serikali mpeleke viwege hiyo hiyo kama ni private mpeleke majority sio wabaya ni wazuri
Sekondari IPO Halisi ni nzuri na inafatiwa na viwege Sekondari kama ni mwanaume unaweza kumpeleka Pugu boy kama kafaulu vizuri (science) pia kama unaweza kulipa nauli kidogo Kila asubuhi mpeleke Juhudi Sec hii ni nzuri zaidi kwenye eneo letu
Karibu sana viwege
 
Viwege ipo pande zipi hapo Dsm
 
Dah, viwege jamani😪😪 kuhusu shule sijui ila umenikumbusha uchungu. Kila la kheri
 
Ahsante mkuu. Wote ni wakike na wapo shule za serikali vilevile kwa hali ilivyo nahitaji kuwapeleka shule ya serikali pia
 
Mdogo mpeleke viwege primary
Mkubwa mpeleke Halisi ukikosa mpeleke viwege sio shule mbaya usimamizi wako ukiwa mzuri wanakupa matokeo mazuri
 
Dah, viwege jamani😪😪 kuhusu shule sijui ila umenikumbusha uchungu. Kila la kheri
Pole sana mkuu, kuna shida gani kiongozi hadi nakukumbusha machungu?
 
Mdogo mpeleke viwege primary
Mkubwa mpeleke Halisi ukikosa mpeleke viwege sio shule mbaya usimamizi wako ukiwa mzuri wanakupa matokeo mazuri
Ahsante mkuu, usimamizi utakuwepo. Ngoja niweke mambo sawa alau niweze kufatilia juu ya shule hizo ulizoniambia mkuu
 
Kama ana ufaulu mzuri na utawezana na nauli unaweza ifikiria na Juhudi yenyewe iko goms ni gari Moja au anapanda train hili eneo ni home of schools hakuna shida ni unajipimia
 
Vipi ni shule ya seerikali ama private?
 
Back
Top Bottom