Msaada kwa anayejua utaratibu wa kumpeleka mtu kwenye wodi ya vichaa

wakifanya hivyo ndio watakuwa wamemsaidia nini hapo ?

mbona unaongea utumbo.
Mkuu humu Kuna vichaa kabisa kama huyu anayeongea utumbo wakati mwenzake ana shida kubwa sana
 
Mpeleke sober house
 
Sasa kati ya yeye nanyie mnayempa mafuta ya mwamposa nani anastahili kutangulia wodi ya vichaa??[emoji3]
Wewe ndio unaonekana kichaa mkuu, suala la mafuta ya Mwamposa ni suala la ki Imani kwamba huenda labda waliamini ndugu Yao amerogwa...

Hivi kumbe kufikiria huwaga ni vigumu eeh?
 
Ukiweza kumsafirisha mpeleke Mloganzila mkuu,
Kuna kitengo cha wagonjwa wa akili, madaktari bingwa wa akili na wodi ya kisasa yenye nyenzo muhimu kwa wagonjwa wa aina hiyo.

Shida ya bangi wapo wagonjwa wengi pale na huwa wanatibiwa na kuruhusiwa wakipata nafuu.Pia ukiruhusiwa kuna utaratibu wa kuhudhuria clinic kwa ufuatiliaji wa mara kwa mara mpaka wahakikishe uko vizuri.

Kuhusu utaratibu ni kwamba unamchukua mgonjwa na kwenda naye hospitali watampokea na kumhudumia ila kama ni wakufanya fujo huwa anapokelewa kitengo cha dharura (emergency department) wanampa huduma ya kwanza na kumpeleka wodini.

Mara nyingi huduma hiyo hutolewa bure( hugharamiwa na serikali).

Pole sana mkuu.


Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Muulize ndugai
 
Poleni sana ... Mpeleke hospitali yoyote ya wilaya au mkoa. Watamtibu Kwa kumpa dawa na/au rufaa kwenda Mirembe. Magonjwa ya akili yanatibika bure tu kama ikithibitika ni ya muda mrefu.
 
Wewe ndio unaonekana kichaa mkuu, suala la mafuta ya Mwamposa ni suala la ki Imani kwamba huenda labda waliamini ndugu Yao amerogwa...

Hivi kumbe kufikiria huwaga ni vigumu eeh?
Mafuta yana kazi gani sasa km sio ukichaa tu..
 
Kazi mnayo, ni kumuomba mungu tu. Wengi wa hao wanaohugua vichaa vya bangi, wakipelekwaga hospital huwa wana behave vizuri na kuonekana wamepona. Wakishatoka baada ya wiki moja ama mbili wanaludi mulemule.
 
Mmekosea, Mwamposa ni msanii tu.....mafuta yake hayaponyi wala kusaidia kitu chochote hana tofauti na wasanii wengine wanaojiita mitume uchwara. Mkamateni ndugu yenu mpelekeni hospitali, atapimwa na ikibainika ni chizi watachukua taratibu sahihi za kuwasaidia.
 
Nipe uzoefu mkuu. Mlimpeleka hospitali?
Yaaan amekaa mloganzila mwezi wanampa dawa wap ...to cut the story tuliamua kurud nae mkoani kwetu nako amekaa mno hospital until anaaga dunia ..kuhusu kwenda milembe tulikataa baada ya ushaur wa wazoefu na hospital hiyo iliyopo dom.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…