msaada wa mawazo yenu ndugu zangu, mdogo wangu ana 4 ya 26 na ana C mbili za english na civic.
Geog ana f, physics, math, chemistry, biology na kiswahli ana D zote.
Nimefikiria kuomba wizara ya afya, elimu na maliasili na utalii ktengo cha misitu, pia nataka kumuombea chuo cha uongozi wa mahakama lushoto.
OMBI LANGU KWENU
Je kuna sehemu au fani nyingne ambazo ninaweza kumpeleka huyu kwa matokeo haya? Naomba sana msaada wenu.
Natanguliza shukrani zangu kwenu.
Nakusihi, hata kama hapendi, umshawishi na umpeleke astashada (certificate) ya afya, inaweza kuwa medical lab au pharmacy, kwa kuwa anakidhi viwango. Itachujua miaka miwili. Huko kwenye Elimu, nahisi mwaka huu wanataka Div. III ya alama 25, huko kwenye utalii sipaami hususani kwenye soko la ajira. Kuwa makini juu ya atakachosoma. Kuna fani nyingi sana ila hazina mustakabali wa maisha.
Ahsante

lushoto kumechafuka ataishia kuwa karani tu ,serikali imeajiri watu 300 mahakimu mahakama za mwanzo,asomee mambo ya pharmacy,vyuo vya kilimo au ufundi na tourisimMpeleke Lushoto ukimpeleka kwengine utampoteza tu.
Yeyw alikuwa na malengo gani?
Yeyw alikuwa na malengo gani?
Uwe makini sana katika kusikiliza machaguo/mapendekezo ya mtoto, ili kujua namna ya kufanya guidance (guidance ni muhimu sana ili kufuta fikra hasi). Nasema hivyo kwa kuwa, wengi wao hawajui mustakabali wa wanayotaka, kwa mfano wengi hupendelea utalii, computer n.k ili hali hawajui ugumu wa kupata kazi. Kuna mdau amependekeza vtuo vya afya, hata mimi naunga mkono, kwani baada ya miaka michache utayaona mafanikio. Kuna rafiki yangu nilimwona ya kwamba wamefeli, kwa kuwa hawakufanikiwa kuingia kidato cha Tano hivyo wakenda vyuo vya afya na kilimo. Kwa sasa wana maisha bora ili hali tuioingia kidato cha Tano na kuhitimu vyuo vikuu tupo hoi bin taabani.
Ndg mmpeleke vyuo vya afya..wizara ya afya huwa wanatangaza nafasi..huko kilimo.utalii utaliaa na kupoteza hela bureeee
.afya kz kibao yeye tu na ujanja wake ajira atapata na kijiwe atafanya
Asome pharmacy inalipa mnoo au co