Msaada kwa Mwalimu huyu; Mikono inatetemeka sababu ya pombe kali. Anashindwa kuweka saini na kusahihisha mitihani. Ipi tiba yake?

Acha pombe mkuu utakufa na kama umeshafikia hiyo hatua,usipoacha pombe anza kuandaa wosia kabla ya huu mwaka kuisha usije acha ugomvi wa mirathi.
 
Acha pombe mkuu utakufa na kama umeshafikia hiyo hatua,usipoacha pombe anza kuandaa wosia kabla ya huu mwaka kuisha usije acha ugomvi wa mirathi.
Kwa kweli amefikia hatua mbaya sana; aanze tu kuandika wosia asije kuacha ndugu wanagombea mali kwa uzembe wake wa kutokuacha wosia.
 
Ni jamaa yangu..kila siku nipo naye kijiweni.

Ila mikono inatetemeka na anashindwa kusaini na kusahihisha madaftali.

Ipi tiba yake?
Fotoa lete picha yake ili tuitathimini na kutoa ushauri wa kumsaidia.
 
Asipokunywa hapati usingizi

Huyo amefikia pabaya anahitaji tiba mbili, kimwili na kiakili

ukosefu wa usingizi ni msongo wa mawazo\stress

huyo anahitaji mapumziko, dawa na ushauri wa kisaikolojia

mtu kama huyo hawezi kuwa na ufanisi kazini, atakuwa mtumwa wa pombe, afya mbovu na kipato duni, madeni na kupoteza nuru ya maisha

msaidie mwenzako mapema kabla ini na figo kuzorota au kufukuzwa kazi
 
Ni jamaa yangu..kila siku nipo naye kijiweni.

Ila mikono inatetemeka na anashindwa kusaini na kusahihisha madaftali.

Ipi tiba yake?
Umeweza kutype vp we mwalimu wa civics?
Acha pombe kali za bei rahisi, ni ww ndo unaomba msaada!
 
Kushika peni kusahihisha au kusaini anashindwa ila kikopo cha kangala akikisha mikono inakuwa stable
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…