Msaada kwa Mwalimu huyu; Mikono inatetemeka sababu ya pombe kali. Anashindwa kuweka saini na kusahihisha mitihani. Ipi tiba yake?

Msaada kwa Mwalimu huyu; Mikono inatetemeka sababu ya pombe kali. Anashindwa kuweka saini na kusahihisha mitihani. Ipi tiba yake?

Hanw mda mrefu uyo kabakiza kreti 3 tu kama ni k vant au konyagi kabakiza 15 tuna fukia
 
Dah!.... hatari hii... DR Mambo Jambo hii ni dalili ya nini?
Kwanza Kabisa Kwa hatua Aliyofikia Ningeshauri aache Kabisa Kunywa Pombe kali na aanze Program ya Alcohol withdraw inasaida wengi sana

Shida aliyonayo kwa sasa ni Alcohol-Induced Tremor (kutokana na acute intoxication):

Hii inatokea kutokana na toxic effects ya alcohol kwenye central nervous system particularly kwenye cerebellum,ambayo ndo ina controls fine motor movements na balance.

Kitu kimoja Kinafaa Tukijue zaidi Chronic alcohol consumption licha ya Ku "damage" liver kama wengi wanavyojua pia Hu "damage" cerebellum over time,ambayo ndo husababisha tremors, Kushindwa Kutembea kwa kunyooka (Unstable Gait), na matatizo ya coordination (ataxia),ndo maana unaweza Kumkuta Mlevi hata kama hajalewa ila hawezi kutembea kwa kunyooka..

Matibabu na Ushauri wangu Ni Kuwa, Ntarudia Tena Ubora kwake yeye ni kuanza Withdraw Program..

Ila hata hivyo itapendeza kama atakunywa maji mengi sana kwa ajili ya Hydration na Detoxification, alcoloh mara nyingi husababisha Dehydration mwilini kwahyo anatakiwa Ajifanyie Program ya KujiHydrate kwa kunywa maji na pia Ajifanyie Detox..


Atafute dawa aina za Beta-blocker sana sana propranolol ambayo inaweza kucontrol alcohol-induced tremors kwa kuzipunguza sympathetic nervous system activity.

Ajitahidi Sana Kutumia Chala.na lishe Bora kwangu mimi Ninge Muongeza Vitamini B suplements kwa sababu lazima atakuwa na lack of Thiamine (Vitamin B1) unajua Chronic alcohol hupelekea matumizi makubwa ya thiamine hivyo kusababisha upungufu mkubwa mwilini..
na kama Unabyojua kazi kubwa ya Thiaminile ni Katika Neurogenerative purpose kwahiyo ikitumika sana inasababibisha neurodegeneration and Wernicke-Korsakoff syndrome. kwa Hiyi Vitamini B au akipata VITA CAP au NAT B itamsaidia sana..

Sana sana NAT B...NA kama akiweza apate na magnesium kwa sababu alcohol hupunguza pia magnesium na ni.madini.Muhimu sana kwa Neurone

Na Ahudhurie Hospitali mara kwa mara kupima na kuangalia hali yake inaendeleaje..
 
Back
Top Bottom