Msaada kwa tatizo la mwanangu

Msaada kwa tatizo la mwanangu

Totos Boss

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2012
Posts
5,456
Reaction score
1,567
Wana jamvi amani iwe kwenu na watanzania kwa jumla.

Mwanangu ana umri wa miaka 3 na mienzi 4 anatatizo la kua hataki/hapendi kula. Nimejaribiu hospitali amemaliza dozi lakini bado, nahitaji kama wataalamu mnazifahamu dawa za kienyeji/miti shamba kwa tatizo hili mnifahamishe.
Natanguliza shukurani kwenu.
 
Kama una uwezo mbadilishie aina tofauti tofauti ya chakula. Kama hapendi ugali mjaribu wali kama hapendi mjaribu pilau..chips au tambi..lazima kuna chakula kati ya hivyo atapenda kula..wakati ukihangaika kutafuta aina ya chakula anachopenda hakikisha unampa matunda au juisi ya matunda..matunda kama parachichi na matikiti hupendwa sana na watoto..pia samaki hupendwa pia na watoto..usitafute mizizi kwanza fanya hivyo hope utapata ufumbuzi wa hilo tatizo
 
mpige piza
burger
kuku
nini
unampa mlo wa aina moja
wali ,ugali wali ugali tambi kachoka hivo vyakula dogo
 
mtafutie mahali ambapo kuna watoto wengi wa umri wake hasa uswazi halafu wawekee chakula wale pamoja kama wiki moja mfululizo halafu utaona matokeo yake

umri kama wake huku kwetu wanapewa dawa za minyoo ili wapunguze kula
 
Wana jamvi amani iwe kwenu na watanzania kwa jumla.

Mwanangu ana umri wa miaka 3 na mienzi 4 anatatizo la kua hataki/hapendi kula. Nimejaribiu hospitali amemaliza dozi lakini bado, nahitaji kama wataalamu mnazifahamu dawa za kienyeji/miti shamba kwa tatizo hili mnifahamishe.
Natanguliza shukurani kwenu.
Inawezekana unandaa chakula safi sana lakini bado mtoto anasumbua kula ili kumbadilisha tabia apende kula unatakiwa kumtengenezea kwanza hamu ya kula maana bila ya kuwa na hamu ya kula hata chakula kiwe kizuri vipi huwezi kula vizuri.

Hamu ya kula inatakiwa kuanzia asubuhi unapofungua kinywa, tengeneza chai iwe ya rangi au ya maziwa weka tangawizi ya unga kwenye nusu lita ya maji au maziwa weka tangawizi kijiko kidogo cha chai mzoweshe mwanao chai hii kila siku asubuhi tangawizi ni kiungo kizuri kinachosaidia kumengenya chakula tumboni na kusababisha njaa haraka na hamu ya kula.

Hapo utakua umemtengenezea mtoto hamu ya kula mchana, kwa kumuandalia mtoto hamu ya kula chakula cha usiku tengeneza juisi ya Pasheni au Embe au Nanasi au tunda lolote lile kumbuka kuchanganya tena kijiko kidogo cha chai kilicho jaa tangawizi na usage pamoja na mchanyanyiko wako mpe mtoto glasi moja saafi kabla ya kula na mabadiliko utayaona usimpatie baada ya kula maana itamsababishia njaa.
 
Kama una uwezo mbadilishie aina tofauti tofauti ya chakula. Kama hapendi ugali mjaribu wali kama hapendi mjaribu pilau..chips au tambi..lazima kuna chakula kati ya hivyo atapenda kula..wakati ukihangaika kutafuta aina ya chakula anachopenda hakikisha unampa matunda au juisi ya matunda..matunda kama parachichi na matikiti hupendwa sana na watoto..pia samaki hupendwa pia na watoto..usitafute mizizi kwanza fanya hivyo hope utapata ufumbuzi wa hilo tatizo
Thanks
 
Back
Top Bottom