Msaada: Kwa Tsh. Milioni 26 naweza kujenga nyumba ya vyumba viwili nchini?

Msaada: Kwa Tsh. Milioni 26 naweza kujenga nyumba ya vyumba viwili nchini?

Inawezekana kama utasimamia mwenyewe na sio kujenga kwa simu na WhatsApp. Na pia kama kiwanja kipo tayri.


KAZI ni kipimo cha UTU
 
Ila usimamie mwenyewe pia upate connection ya kununua material kwa bei nzuri. Town usipokuwa makini mafundi na mawinga ni shida
 
Nyumba ndogo kabisa room mbili na sebule
 
Nipe m 15 tuandikishane kwa mwanadheria nikukabidhi vyumba vyako viwili mkuu
 
Ila usimamie mwenyewe pia upate connection ya kununua material kwa bei nzuri. Town usipokuwa makini mafundi na mawinga ni shida
Yaani ni balaa! Kuna jamaa alienda na fundi kununua nyaya za umeme alipigwa na kitu kizito nyaya zote 1.5 na 2.5 aliuziwa kwa bei linganifu 100,000/= na alichukua za kutosha mwisho wa siku akafanya uchunguzi kwenye maduka akagundua 1.5 ilikuwa inauzwa kwa range ya 50000/= hadi 55000/=. hapo keshapigwa.

Bado fundi huyo huyo akafanya mbinu nyingine ya kutaka amuibie tena boss wake akakamatwa na jaribio likawa limefeli, Kiukweli umakini unahitajika sana.
 
Wakuu.

Hivi kwa milioni 26 za Kitanzania unaweza kujenga nyumba ya vyumba viwili, sitting room, jiko na choo na ikaisha full kuhamia.
Mimi sio fundi ila kwa uzoefu naona utafikia hatua nzuri na vitabakia vitu vichache sana. Kwa makadirio yasiyo rasmi ukiwa na hesabu hiyo utaweza:-

Kuinua boma chukulia 6.5M
Tofali 2400
Sementi 35 hadi 40 bags
Mchanga tripu 2 za Mende
Kokoto tripu moja tipa ya kawaida.
Nondo
Binding wire
Mbao kwa ajili ya mkanda na renta.
Ufundi.

Kupaua chukulia 5.5M
Kuweka magrill yote chukulia 1.5M
Kupiga plaster nje na ndani chukulia 1.5
Kuweka miundombinu ya umeme. chukulia 2.2M (Tanesco+complete wiring +ufundi) kama huitaji nguzo
Kuweka milango ya mbao kama una milango 6 chukulia 2M.
Skimming nje na ndani chukulia 1.5M
Blandering na kufunga gypsum board chukulia 1.2M
Kupaka rangi chukulia nje na ndani tuipe 1M.
Tiles tuipe 1M
Shimo la choo kuchimba na kujenga chukulia 1.5M
Masink ya vyoo na mifumo ya maji tuipe 500K
Aluminium tuipe 2M.


Mengineyo.
Urembo.
Mapazia na fimbo zake.
Choo cha nje
Hakuna fensi.
Hakuna kitchen cabinet.
 
Back
Top Bottom