Wakuu.
Hivi kwa milioni 26 za Kitanzania unaweza kujenga nyumba ya vyumba viwili, sitting room, jiko na choo na ikaisha full kuhamia.
Mimi sio fundi ila kwa uzoefu naona utafikia hatua nzuri na vitabakia vitu vichache sana. Kwa makadirio yasiyo rasmi ukiwa na hesabu hiyo utaweza:-
Kuinua boma chukulia 6.5M
Tofali 2400
Sementi 35 hadi 40 bags
Mchanga tripu 2 za Mende
Kokoto tripu moja tipa ya kawaida.
Nondo
Binding wire
Mbao kwa ajili ya mkanda na renta.
Ufundi.
Kupaua chukulia 5.5M
Kuweka magrill yote chukulia 1.5M
Kupiga plaster nje na ndani chukulia 1.5
Kuweka miundombinu ya umeme. chukulia 2.2M (Tanesco+complete wiring +ufundi) kama huitaji nguzo
Kuweka milango ya mbao kama una milango 6 chukulia 2M.
Skimming nje na ndani chukulia 1.5M
Blandering na kufunga gypsum board chukulia 1.2M
Kupaka rangi chukulia nje na ndani tuipe 1M.
Tiles tuipe 1M
Shimo la choo kuchimba na kujenga chukulia 1.5M
Masink ya vyoo na mifumo ya maji tuipe 500K
Aluminium tuipe 2M.
Mengineyo.
Urembo.
Mapazia na fimbo zake.
Choo cha nje
Hakuna fensi.
Hakuna kitchen cabinet.