Msaada kwa Ugonjwa huu wa kuku

Msaada kwa Ugonjwa huu wa kuku

Deontic

Member
Joined
Aug 26, 2020
Posts
14
Reaction score
7
Vifaranga wangu 20 wa miezi miwili wanatoa kinyesi laini cheupe na wanakosa nguvu ya kusimama, miguu inalegea pia wamezubaa, naombeni ushauri ni dawa gani inafaa niwanusuru , maana mpaka sasa kafa mmoja na watano wanahali mbaya hawali kabisa, pia wanatoa kinyesi chenye maji maji.
View attachment 2348634
 
Jitahidi basi mkuu ukifika AGROVET utapata chanjo sahihi maana ufugaji una changamoto
Shukrani but nitumie chanjo ipi maana kuna vifaraga wengine 30 wana wiki moja sijawapa chanjo yoyote na je naweza kuwachanja wote hata wanaoumwa?
 
Shukrani but nitumie chanjo ipi maana kuna vifaraga wengine 30 wana wiki moja sijawapa chanjo yoyote na je naweza kuwachanja wote hata wanaoumwa?
Kifaranga wa wiki moja angestahili ukute anapata chanjo ya 3 sasa ambayo ni ya kideri na mbili zilizopita ni za Marek's na Pulorum
 
Kuna dawa ile ya madini ya calcium kama sijakosea ndio tiba yake.
Ni ungaunga, ukipata kopo moja la elfu 5 unatibu hata kuku elfu 1 na zaidi
 
Hawakupewa chanjo japo wakubwa nao walipewa mwezi wa saba nilitaka nirudie tena mwezi kumi
Aiseee chanjo ni muhimu sana acha kufuga kwa hasara na kuja kulia lia jukwaani, chanjo ni muhimu kama maji, chakula na usafi wa banda. Hayo mambo zingatia wakati wote.
 
Back
Top Bottom