Msaada kwa wenye viwanja mjini DAR, ninahitaji kununua eneo

Msaada kwa wenye viwanja mjini DAR, ninahitaji kununua eneo

SEASON 5

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
481
Reaction score
1,008
Ndugu zangu maisha haya kuna wakati inatakiwa mtu ukubali tu kuna waliokutangulia na ujishushe uombe msaada wao na ndicho ninachokifanya hapa kwenu ndugu zangu, nimejitahidi katika kuhangaika na maisha huku na kule vibarua na viajira nimepata kiasi cha 1M nimekuja kwenu ndugu zangu wenye viwanja vikubwa vikubwa ambavyo mnavitumia lakini kuna nafasi imebaki ya kujenga hata chumba na sebule na choo tu basi inantosha naomba mnimegeee kakisehemu ndugu yenu.

Yawezekana una eneo kubwa sana limepimwa lipo tu naomba basi nimegee kasehemu kadogo tu namimi nijijengee narum kamoja kasebule na chooo yani hata sihitaji uwanja mkubwa nahitaji kasehemu kakupumzika kuepuka kodi za mwisho wa mwezi, huko mbeleni nikipata hela namimi ntanunua kiwanja changu kikubwa ila kwasasa naomba mnisaidie kaeneo kadogo tu nijihifadhi ndugu yenu.

Nina 1m (millioni moja) sina kitu naomba msaada wenu wenye viwanja vikubwa vikubwa maeneo ya mjini yasio mbali na barabara ,nipo chini yenu nanyenyekea naomba msaada wenu.

ASANTENI.
 
Kipo mkuu,
Tena mjini kabisa.

Kiko Morogoro ROAD,
Kimetizamana na geti kuu la kuingia OFISI za makao makuu ya MWENDO KASI.

Yaan ni hatua 2 uko RAMi ya Morogoro road.

Kwa maelezo zaidi nichek PM
 
Unataka kupewa msaada au unataka ununue eneo kwa milioni moja?

N.B kupewa msaada ni kutoa ela na kumegewa eneo tu bila utaratibu.
Kununua kiwanja ni pamoja na kuandikishana ili ionekane kasehemu hako ulichomegewa ni mali yako halali.
 
Unataka kupewa msaada au unataka ununue eneo kwa milioni moja?

N.B kupewa msaada ni kutoa ela na kumegewa eneo tu bila utaratibu.
Kununua kiwanja ni pamoja na kuandikishana ili ionekane kasehemu hako ulichomegewa ni mali yako halali.
Naomba kupewa msaada ambapo ni kununua pia hako kasehemu kadogo nitakachomegewa kawe ni mali yangu bila masharti yeyote lakini hili ni ombi mkuu,kama wahusika wapo wanisaidie.
 
Back
Top Bottom