Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,663
- Thread starter
-
- #41
Hali kama yako ilinikosesha kazi sehemu nyingi sana, nikiingia kwenye interview nilikua natetemeka nusu kufa.. jamaa wakiangalia vyeti nilivopasua wanashangaa ile mbaya
nikaanza kwenda shule flani flani nawafundisha watoto..
kwa sasa naweza kuhutubia hata watu 500 bila kuogopa.. pia ni muongeaji mzuri..nimekua kiongozi sehemu mbalimbali.. ndugu utakosa fulsa.. jitutumue.. tatizo ni kulelewa na wazazi wababe.. mimi baba yangu alikua mtu wa ajabu sana.
Kumbe tupo wengi. Hata mimi nina tatizo hili. Nimekuwa nalo tangu nikiwa shule ya msingi. Nilikuwa bright darasani, lakini ilipokuwa ikifika mwalimu akaninyanyua nisome hata aya moja kwenye kitabu cha kiswahili nilikuwa nashindwa kabisa. Siku moja alikuja mwalimu wa kiswahili mgeni--alihamia shuleni kwetu--akaniambia nisome (tulikuwa tukisoma kwa zamu--kwa wale wanafunzi mliosoma miaka ya 80's mnafhamu hili). Nilishindwa kabisa. Basi siku hiyo aliporejea Staff room, akawauliza walimu inakuwaje mwanafunzi wa drs la sita asijue kusoma. Wakamuambia mimi ndiye genius darasani ila hiyo habari ya kusoma vitabu darasani siiwezi kabisa. Bado hali hiyo ninayo mpaka leo. Kujieleza mbele ya kikundi cha watu 5 au 6 ni shida sana, hasa pale ninapokuwa nimechukua nafasi ya main speaker huku watu wote wakinitazama na kunisikiliza--points zote nilizokuwa nataka kuongea huyeyuka na kijasho jembamba huanza kunitoka.
na ukiwa unapiga gemu dushelele nayo inavibrate au....Habari wapendwa!
Hili tatizo la kutetemeka wakati ninapowasiliana na wengine sijui litaisha lini.
Maana ni aibu sana nashindwa kuwasilisha hoja zangu makini sababu ya kutetemeka.
Pumzi zinaisha kabisa na nahisi moto unaniwakia ninapotaka kuongea!!
Yaani nashindwa nifanyeje japokua ni suala muhimu kwangu inabidi nikae kimya ili nisijetetemeka"
Nikiongea naona najichanganya sababu ya kupanic!
Kwa anaemjua Dr yoyote wa Saikolojia mjini Arusha naomba mnisaidie na Ushauri pia.
NB:Moderator Paw Invisible
Msiupeleke huu uzi jukwaa la Doktar.
Mkuu umesema vema.Mkuu sifikri kama kuna dawa ya kukufanya usitetemeke ila ni swala la kisaikolojia zaidi nafikiri ukimuona daktari wa saikolojia atakusaidia,hebu jaribu Seliani ile ya mjini acha ile ya Ngaramtoni.
Lakini njia yenyingine kupunguza hilo ni kuelewa kwa ufasaha kile unacho present inapunguza hofu.
Mimi nilikuwa na tatiza hilo mimi liliisha kwa kumuomba Mungu sana maana ilifikia hatua hata nikiongea mbele ya watu 6 natetemeka lakini sasa naongea hata kwa maelfu.
Hili ni tatizo kwa watu wengi sana nakumbuka nikiwa chuo kuna jamaa walikuwa wanatumia viroba ndio wanafanya presentation.
Huwa nnapata wakati mgumu pale ninapoongea halafu watu wote wakawa wananiangalia mimi yaani hii siipendi nahisi kama macho yao yananitoboa.
Kingine sipendi kuangaliwa usoni .
Na nnapoongea sipendi ile hali kama watu hawajaelewa kwa hio wanataka urudie hapo ndio nachanganyikiwa na kupanik pumzi zinaisha mpaka bassss
Sijaelewa kama tatizo lako kuu ni hofu ya kuzungumza mbele za watu, na hivyo kutetemeka na kukosa pumzi au ni kutetemeka hata pale unapokuwa peke yako (e.g unajibu msg kwa simu au laptop). Kama ni hilo la kwanza with time na kwa kulifanyia mazoezi waweza kulimaliza, kwani ni kawaida ya wengi kuwa na hofu pale anapofanya presentation, hata kama ni mbele ya watu wachache (kuna exceptions za watu wanaozaliwa na uwezo wa kujieleza) na ndiyo maana watu wote makini (hata akina Obama) huwa wanafanya rehersal ya atakachokiwa. Zamani kwenye mashule ya sekondari kulikuwa na kitu kinaitwa debate clubs ambazo zilisaidia sana vijana kujifunza namna ya kujieleza na kujenga hoja. Hivyo ili uondokane na tatizo hilo ni lazima ujichanganye kwenye mijadala lakini anza na ile unayoielewa vizuri, kwani hofu hii huchangiwa pia na kutoijua/kutoimudu mada yako vizuri.Ni kama mtu anayeingia kwenye chumba cha mtihani akiwa amejiandaa vya kutosha atakuwa at easy as compared na ambaye hajajiandaa.
Mi sipendi kabisa nikiongea mtu aniangalie machoni yaani basi tu !!"""
basi usije kutana na mie, nna.tabia.mbaya ya kumtizama mtu kati kati ya mboni.
Da ndg pole sana una tatizo km langu, mi niko chuoni yaani cku za presentation kwangu huwa ni balaa, nimeshajaribu kuomba ushauri humu jf lkn pamoja na shauri mbalimbali nzuri lkn tatzo bado linanitafuna.
Wkt mwngne hata lecturer akiwa anafndsha ile anapouliza swali akikuangalia tu hofu na kutetemeka kuna tamalaki hata kitu nakifahamu nakuwa na wasiwasi ajabu, na drs langu tuko wachache kiasi kwamba lazma utaongea tu!
Hahahahahahaha! Mkuu, nimecheka sana--si unajua tena viroba vinaua soo?
nakumbuka jamaa alikunywa viroba badala atoe conclution akaanza tena introduction..
Tell yourself, "relax, you are good"
Take deep breath
Habari wapendwa!
Hili tatizo la kutetemeka wakati ninapowasiliana na wengine sijui litaisha lini.
Maana ni aibu sana nashindwa kuwasilisha hoja zangu makini sababu ya kutetemeka.
Pumzi zinaisha kabisa na nahisi moto unaniwakia ninapotaka kuongea!!
Yaani nashindwa nifanyeje japokua ni suala muhimu kwangu inabidi nikae kimya ili nisijetetemeka"
Nikiongea naona najichanganya sababu ya kupanic!
Kwa anaemjua Dr yoyote wa Saikolojia mjini Arusha naomba mnisaidie na Ushauri pia.
NB:Moderator Paw Invisible
Msiupeleke huu uzi jukwaa la Doktar.