Msaada kwanini natetemeka sana?

Msaada kwanini natetemeka sana?

Hali kama yako ilinikosesha kazi sehemu nyingi sana, nikiingia kwenye interview nilikua natetemeka nusu kufa.. jamaa wakiangalia vyeti nilivopasua wanashangaa ile mbaya
nikaanza kwenda shule flani flani nawafundisha watoto..
kwa sasa naweza kuhutubia hata watu 500 bila kuogopa.. pia ni muongeaji mzuri..nimekua kiongozi sehemu mbalimbali.. ndugu utakosa fulsa.. jitutumue.. tatizo ni kulelewa na wazazi wababe.. mimi baba yangu alikua mtu wa ajabu sana.

Unayosema ni kweli.
Upande wa wazazi hasa baba alikua mkali sana!
 
Kumbe tupo wengi. Hata mimi nina tatizo hili. Nimekuwa nalo tangu nikiwa shule ya msingi. Nilikuwa bright darasani, lakini ilipokuwa ikifika mwalimu akaninyanyua nisome hata aya moja kwenye kitabu cha kiswahili nilikuwa nashindwa kabisa. Siku moja alikuja mwalimu wa kiswahili mgeni--alihamia shuleni kwetu--akaniambia nisome (tulikuwa tukisoma kwa zamu--kwa wale wanafunzi mliosoma miaka ya 80's mnafhamu hili). Nilishindwa kabisa. Basi siku hiyo aliporejea Staff room, akawauliza walimu inakuwaje mwanafunzi wa drs la sita asijue kusoma. Wakamuambia mimi ndiye genius darasani ila hiyo habari ya kusoma vitabu darasani siiwezi kabisa. Bado hali hiyo ninayo mpaka leo. Kujieleza mbele ya kikundi cha watu 5 au 6 ni shida sana, hasa pale ninapokuwa nimechukua nafasi ya main speaker huku watu wote wakinitazama na kunisikiliza--points zote nilizokuwa nataka kuongea huyeyuka na kijasho jembamba huanza kunitoka.

Hili ni tatizo kwa watu wengi sana nakumbuka nikiwa chuo kuna jamaa walikuwa wanatumia viroba ndio wanafanya presentation.
 
Habari wapendwa!

Hili tatizo la kutetemeka wakati ninapowasiliana na wengine sijui litaisha lini.

Maana ni aibu sana nashindwa kuwasilisha hoja zangu makini sababu ya kutetemeka.

Pumzi zinaisha kabisa na nahisi moto unaniwakia ninapotaka kuongea!!
Yaani nashindwa nifanyeje japokua ni suala muhimu kwangu inabidi nikae kimya ili nisijetetemeka"

Nikiongea naona najichanganya sababu ya kupanic!

Kwa anaemjua Dr yoyote wa Saikolojia mjini Arusha naomba mnisaidie na Ushauri pia.
NB:Moderator Paw Invisible
Msiupeleke huu uzi jukwaa la Doktar.
na ukiwa unapiga gemu dushelele nayo inavibrate au....
 
Hayo ndo yalimkuta Mh Mulugo. Unahitaji mazoezi ya kuongea na public, jitahidi kufanya mala kwa mala itaisha kadri unavyo panda jukwaani. Anza na idadi ndogo unaendelea isiwe mwoga.
 
Mkuu sifikri kama kuna dawa ya kukufanya usitetemeke ila ni swala la kisaikolojia zaidi nafikiri ukimuona daktari wa saikolojia atakusaidia,hebu jaribu Seliani ile ya mjini acha ile ya Ngaramtoni.

Lakini njia yenyingine kupunguza hilo ni kuelewa kwa ufasaha kile unacho present inapunguza hofu.

Mimi nilikuwa na tatiza hilo mimi liliisha kwa kumuomba Mungu sana maana ilifikia hatua hata nikiongea mbele ya watu 6 natetemeka lakini sasa naongea hata kwa maelfu.
Mkuu umesema vema.
Naomba huyu mleta mada ajiamini,ili uanze kujiamini anza kuzungumzia vitu ambavyo una uhakika navyo,punguza story za kusimuliwa ambazo hujui undani wake.Na kama unafanya presentation jijengee kujiamini hata kama ataingia mtu mwenye uelewa zaidi yako akilini mwako jijengee kuwa naye ni mwanafunzi wako,hii itakusaidia kujenga kujiamini.
Lkn ninkukumbushe jitahidi kuanza na vitu ambavyo una uhakika navyo kupunguza kuulizwa maswali ambayo hutakuwa na uwezo wa kkuyajibu na hivyo ikakuongezea hofu.
 
Hili ni tatizo kwa watu wengi sana nakumbuka nikiwa chuo kuna jamaa walikuwa wanatumia viroba ndio wanafanya presentation.

Hahahahahahaha! Mkuu, nimecheka sana--si unajua tena viroba vinaua soo?
 
Huwa nnapata wakati mgumu pale ninapoongea halafu watu wote wakawa wananiangalia mimi yaani hii siipendi nahisi kama macho yao yananitoboa.

Kingine sipendi kuangaliwa usoni .
Na nnapoongea sipendi ile hali kama watu hawajaelewa kwa hio wanataka urudie hapo ndio nachanganyikiwa na kupanik pumzi zinaisha mpaka bassss

Sijaelewa kama tatizo lako kuu ni hofu ya kuzungumza mbele za watu, na hivyo kutetemeka na kukosa pumzi au ni kutetemeka hata pale unapokuwa peke yako (e.g unajibu msg kwa simu au laptop). Kama ni hilo la kwanza with time na kwa kulifanyia mazoezi waweza kulimaliza, kwani ni kawaida ya wengi kuwa na hofu pale anapofanya presentation, hata kama ni mbele ya watu wachache (kuna exceptions za watu wanaozaliwa na uwezo wa kujieleza) na ndiyo maana watu wote makini (hata akina Obama) huwa wanafanya rehersal ya atakachokiwa. Zamani kwenye mashule ya sekondari kulikuwa na kitu kinaitwa debate clubs ambazo zilisaidia sana vijana kujifunza namna ya kujieleza na kujenga hoja. Hivyo ili uondokane na tatizo hilo ni lazima ujichanganye kwenye mijadala lakini anza na ile unayoielewa vizuri, kwani hofu hii huchangiwa pia na kutoijua/kutoimudu mada yako vizuri.Ni kama mtu anayeingia kwenye chumba cha mtihani akiwa amejiandaa vya kutosha atakuwa at easy as compared na ambaye hajajiandaa.
 
Kumbuka Obama yeye hutoa tu hali ya mambo ilivyo lakini hakuna anayemuuliza papo hapo.
 
Da ndg pole sana una tatizo km langu, mi niko chuoni yaani cku za presentation kwangu huwa ni balaa, nimeshajaribu kuomba ushauri humu jf lkn pamoja na shauri mbalimbali nzuri lkn tatzo bado linanitafuna.
Wkt mwngne hata lecturer akiwa anafndsha ile anapouliza swali akikuangalia tu hofu na kutetemeka kuna tamalaki hata kitu nakifahamu nakuwa na wasiwasi ajabu, na drs langu tuko wachache kiasi kwamba lazma utaongea tu!

Hyo ni spirit ya hofu
Bila Mungu happ hutoki!

Kuna wakui happ walinga'ang'ana na Mungu wako ok!
 
hauna confidence ndugu jitahidi kuwa chaming na uwe una interaction za hapa na pale na marafiki walochangamka
 
nakumbuka jamaa alikunywa viroba badala atoe conclution akaanza tena introduction..

hahahahahahaaaaaaaaaaaaaa! mkuu usinivunje mbavu! hii kali sana i see! ni shidaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Habari wapendwa!

Hili tatizo la kutetemeka wakati ninapowasiliana na wengine sijui litaisha lini.

Maana ni aibu sana nashindwa kuwasilisha hoja zangu makini sababu ya kutetemeka.

Pumzi zinaisha kabisa na nahisi moto unaniwakia ninapotaka kuongea!!
Yaani nashindwa nifanyeje japokua ni suala muhimu kwangu inabidi nikae kimya ili nisijetetemeka"

Nikiongea naona najichanganya sababu ya kupanic!

Kwa anaemjua Dr yoyote wa Saikolojia mjini Arusha naomba mnisaidie na Ushauri pia.
NB:Moderator Paw Invisible
Msiupeleke huu uzi jukwaa la Doktar.

Nakumbuka wakati nikiwa shule ya msingi nilikuwa nashindwa kabisa kusoma kitabu darasani hadi walimu wakawa wananishangaa wakati kwenye mitihani nilikuwa naongoza. Hili tatizo la kutoongea hadharani ni balaa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom