Msaada: Mabaka haya kwenye korodani dawa yake nini?

Msaada: Mabaka haya kwenye korodani dawa yake nini?

Kama picha inavyoonekana hapo, nasumbuliwa na hayo mabaka kwenye kende hapo. Vinawasha hatari sio poa.
Msaada wenu dawa gani inafaa?

View attachment 1267366
Hiyo ni 'fungus' nami iliwahi nikamata nchi za joto, lakini nilishasahau dawa gani ilinisaidia, maana ni muda mrefu umepita.

Huduma ya kwanza hapo ni kunyoa mfululizo usiruhusu vuzi kustawi, kisha 'aplai' ushauri wa daktari.
Madawa ya 'tube' ya kupaka yapo kila sampuri utapona, pole.
 
Tumia grisuflavin, ama asufluvin kwa muda wa siku 14 kidonge kimoja kila siku. Pia nunua ointment upake muda wote utakaokuwa unakunywa dawa ointment unapaka asubuhi na jioni ukimaliza kuoga. Hakikisha usafi wa mwili na nguo za ndani. Kama upo Dar usivae nguo nzito ama vijaladio
 
Hii kutibu ni rahisi.Nyoa vizuri oga kwa Detto ya maji na maji yawe ya moto.Then paka maji ya limao vaa boxer piga kazi.

Unapolala pia Fanya hivyo. Baada ya wiki njoo tupe mrejesho
 
Nenda duka la dawa kanunue SEPTRIN za elfu moja ni vidonge kumi utapewa.

Kisha nenda dukani kanunue mafuta ya kupaka aina ya BABYCARE ya kwenye kikopo kidogo kuliko yote bila shaka kina ujazo wa 25g na kinauzwa shilingi mia tatu.

Baada ya kununua hivyo vitu nenda nyumbani chukua vidonge vyako vyote kumi vya SEPTRIN visage viwe unga kabisa. Kisha changanya na hayo mafuta ya BABYCARE hakikisha unachanganya vizuri kabisa mkorogo wako.

Baada ya hapo oga vizuri jikaushe vizuri hizo korodani zako jipake mara mbili kwa siku yaani ASUBUHI NA JIONI. Endelea kupaka kwa siku kumi na nne (wiki mbili).

Na kuhakikisha mabadiliko utaanza kuyaona baada ya siku mbili tu DAWA HII NI YA UHAKIKA.

NOTE: usije changanya hiyo dawa na losheni. NARUDIA TENA USIJE CHANGANYA HIYO DAWA NA LOSHENI.

#usisahau kuleta mrejesho hapa.
 
Sekondari tulikuwa tukiita P.E yaani Pumbu erosion.
Hujifuti maji vizuri ukakauka Mkuu ila pia hutegemea aina ya maji unayooga.
 
Hizo ni fangasi..nenda hospitali.usijaribu kutumia dawa bila ushauri wa dakitari. pia acha kuoga maji yenye chimvi chumvi pamoja na kuvaa boxer inayobana sana.
hapo kweny chumvichumvi umelenga kabis coz mie baharia
 
Back
Top Bottom