Wakuu hiyo kitu inanitesa sana, nimetumia sonadem sana pamoja na intraconazole lakin siponi. Inapotea kwa muda mchache nisipotumia dawa hali inajirudia. Mwenye tiba ya kudumu tafadhari msaada wako unahitajika sana
Hiyo ni chronic fungal infection. Inasababishwa mara nyingi na unyevu wa mara kwa mara wa meneo hayo, na pia hali ya uchafu kama vile kutumia boxer moja kwa muda mrefu bila kubadilisha, hasa maeneo yenye joto kama Dar.
Matibabu:
1.Kitu kikubwa cha kwanza, kabla ya matibabu yoyote yale ni kuzingatia usafi wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na kutovaa boksa kwa zaidi ya siku moja hasa kwa maeneo yenye joto kama Dar, pamoja na kuhakikisha kuwa unapomaliza kuoga, umejifuta vyema maeneo hayo, na pia unapomaliza kujitawaza kwa maji baada ya haja kubwa, unajifuta majimaji na taulo au toilet paper na kuhakikisha kuwa maeneo hayo ni makavu kabisa.
2.Pili, kama unatumia chupi, nashauri uachane na chupi uwe unatumia boksa ambazo ni pana, zinapitisha hewa na ni za COTTON kwa 100% (hizi ni expensive zaidi, but ndizo ambazo zinashauriwa kiafya kwa usalama wa nyeti zako).
3.Tatu, wakati unatumia dawa, hakikisha kwamba boksa zako zote umeziloweka kwenye maji ya moto kabisa kwa muda wa dakika 15-20 kisha uzifue kwa sabuni, na kuzianika kwenye JUA, halafu kabla ya kuzivaa tena uzipige pasi vizuri.
4.Usivae boksa mbichi au yenye unyevu, pia hakikisha boksa zako unazianika kwenye JUA (sio ndani chini ya kitanda); Na hakikisha UNAPIGA PASI boksa kabla hujaivaa.
5.Kama una mpenzi wako ambae mnakutana kimwili, hakikisha pia na yeye anatumia dawa KABLA hujakutana nae tena (dawa za fungus za sehemu za siri kwa wanawake ni tofauti); Otherwise, utajitibu wewe, halafu ukirudi tena kwa mpenzi/mke wako, anakuambukiza tena, fungus zinarudi tena UPYA! Haya maelezo niliyokupatia ni muhimu sana ukayafahamu na ukayafuata,kabla na wakati unakunywa dawa, la sivyo kila siku wewe utakua ni mtu wa kunywa dawa za fungus.
Pole sana
wa ukwee