Msaada: Mafao yameingia kwenye account ya mahakama ya wilaya Temeke, tumezungushwa mpaka tumechoka

Msaada: Mafao yameingia kwenye account ya mahakama ya wilaya Temeke, tumezungushwa mpaka tumechoka

Jembemtaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2014
Posts
1,193
Reaction score
926
Habari ndugu,

Tulikuwa na ndugu yetu alistaafu mwaka 2019 alikua nurse Muhimbili Hospital.

Baada kustaafu alifuatilia mafao yake hakufanikiwa kupata. Baadae akaugua akafa 2020, baada ya kufa tunafungua na tukafanikiwa kuingiziwa mafao kwenye hiyo account ya mahakama.

Cha kusikitisha ni kwamba wanatoa hoja tofauti kila tukitaka kuchukua hiyo hela mpaka msimamizi wa mirathi amekata tamaa.

File wanadai halionekani, mara karani amefiwa, mara mhasibu yuko likizo, mara hakimu hayupo.

Naomba msaada kwa mwenye ufahamu kwenye jambo hili tunaweza kwenda wapi kupata msaada.
 
Back
Top Bottom