Msaada: Mafao yameingia kwenye account ya mahakama ya wilaya Temeke, tumezungushwa mpaka tumechoka

Msaada: Mafao yameingia kwenye account ya mahakama ya wilaya Temeke, tumezungushwa mpaka tumechoka

Mafao ya ndugu yetu yameingizwa kwenye account ya mahakama ya temeke, ivo tumekua tunazungushwa mpaka tumekata tamaa. File limepotea,mara kalani kafiwa, mara mhasibu yuko likizo, mara kuna kikao yaani ni shida.
Umepewa hiyo namba wewe kesho ukiamka asubuhi piga hiyo namba kisha eleza tatizo lako mkuu utasaidiwa.
 
Mafao ya ndugu yetu yameingizwa kwenye account ya mahakama ya temeke, ivo tumekua tunazungushwa mpaka tumekata tamaa. File limepotea,mara kalani kafiwa, mara mhasibu yuko likizo, mara kuna kikao yaani ni shida.
Mkuu mwenye kukusaidia sio mm ndio maana nikakupa hiyo namba ni ya mahakama kitengo maalumu, Piga ueleze Shida yako utasaidika bure
 
We jamaa 🙄🙄🙄🙄
Ongeeni nao, kwamba hela imeingia milioni kadhaa katika hiyo wachukue chao then wawape zenu, hivyoooo
Waongee nao ili iweje? Wanalipwaje pesa kwa kutimiza wajibu wao?

Ndo tatizo la wananchi wengi kutokujua sheria wala taratibu japo kidogo. Watumishi wengi kwenye idara za serikali wakishakuona ww ni kiazi watakusumbua sana.

Mtoa mada,mimi nipo idara ya mahakama ushauri wangu kwako usitoe rushwa wala usiahidi chochote kwa hao watumishi. Kuhudumiwa ni haki yako ya msingi.

Fanya utafiti ulijue jina la hakimu anayesimamia kesi ya mirathi,jina la karani wa mahakama,na jina la muhasibu.

Andika barua ya malalamiko,barua ieleze tatizo lilivyo orodhesha majina ya wahusika namba ya kesi ni muhimu. Apa pia itategemea je,hukumu ya mirathi ilishatoka? Kama imetoka na mnayo mkononi shida itakuwa kwa muhasibu wa mahakama.

Kuna dawati la malalamiko la mahakama wasilisha barua hapo au laah mtafute afisa utumishi wa mahakama ya wilaya ya temeke umkabidhi malalamiko yako, nakala nyingine itume kwa hakimu mkazi mfawidhwi wa mahakama ya mkoa pale kisutu.

Kuna mdau amekupa namba apo juu hiyo namba pia inapatikana kwenye mabango yaliyobandikwa mahakaman ni kwa msaada zaidi. Tatizo wananchi wengi ni waoga na sio wadadisi.

Tatizo lako ni simple tu na linatatulika na kwa kukusaidia watumishi wa mahakama tuna vitambulisho ambavyo tunavivaa kifuani ili iwe rahisi kunote majina ya watumishi wasumbufu.

Achana na wadau hapo juu wanakushauri utoe rushwa. Mtu anayetoa rushwa hana tofauti na asiyejielewa huwezi kutoa rushwa kama unajua haki zako,kuhudumiwa ni haki yako ya kikatiba. Kutoa rushwa kwa kisingizio cha kuepuka usumbufu hakina mantiki. Unaweza kupata haki yako bila usumbufu ikiwa :
1.Unajiamini
2.Unafata maelekezo na taratibu unazopewa
3.Unajua haki zako kama mteja.

Zingatia: Malalamiko yawe kwa maandishi. Mfumo wa mawasiliano mkuu wa kimahakama na serikalini kwa ujumla ni maandishi usiende kulalamika kwa mdomo.

Jitahidi kujieleza vizuri wakati mwingine sababu ya uoga unashindwa kujieleza vizuri ukaeleweka.
 
Binafsi nimekuja kujua maisha ya mwajiriwa hayana Tofauti na mkulima. Unateseka mpaka unakuja kufa. Yaani Nina miaka kadhaa nafanya kazi Ila nakwepa dhana ya kutunziwa hela.

Yani mktaba wa kutunziwa hela huwa nakataa kazi hiyo. Na Tena mpaka ufike 60yrs mbona wabunge wao hawawatunzii. Wewe ndiye wanayekupenda Maana uko Kama mtoto hujui kujiwekea akiba
 
We jamaa [emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
Ongeeni nao, kwamba hela imeingia milioni kadhaa katika hiyo wachukue chao then wawape zenu, hivyoooo
Kwani hao wafanyakazi wa hiyo Mahakama ni warithi pia hadi nao wapewe fungu lao!? Umasikini ni kitu kibaya sana,unakufanya unakua na rohoo ya chuki hadi unakua hutaki kuona ya wenzako yanaenda bila shida, mwenye haki yake apewe na wala haina haja ya kumcheleweshea!!
 
Ushauri wa wengi unaonesha jinsi TZ wanavyo ipalilia rushwa. Kwaakili za wrngi rushwa haitapungua wala kuisha.
 
Usipojiongeza utakoma. Mi nilikuwa na tatizo fulani hivi kweny hii mitandaon yetu kwakweli nilizunguka kufuatilia kwa zaidi ya miezi miwili. Jana nikaenda ofisini baada ya salam nikamwambia "sema nijiongeze vipi maana najua hili tatizo si la kuchukua muda mrefu hivi,sema nifanyaje?" Akajibu acha 20K niliiacha jion ananipigia simu nimekamilisha
 
Back
Top Bottom