Msaada: Majibu ya vipimo vya UTI kufotautiana ndani ya lisaa limoja nini tatizo

Msaada: Majibu ya vipimo vya UTI kufotautiana ndani ya lisaa limoja nini tatizo

Lee

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
43,973
Reaction score
150,463
Wiki kadhaa nilikuwa nasumbuliwa na UTI baada ya kupata vipimo katika kituo cha afya X na doctor akanishauri nitumie dawa make alisema sio nyingi ni ya kawaida ..baada ya kumaliza dozi ikabidi nirudi kujiridhisha kama nimepona ugonjwa ila cha ajabu majibu yakatoka kuwa nina UTI ya kutosha kwa maelezo ya doctor kuwa dawa hazijasaidia akashauri nichome sindano katika hicho kituo cha afya X..majibu yake kama hivi.

20211102_065419.jpg

Ila nikaona nisikurupuke nikiwa njiani nikapata wazo la kwenda kujiridhisha katika kituo cha afya Y kingine na kumsikiliza docter means kwa kupima tena ambapo nilitumia mda wa lisaa limoja majibu ya pili kutoka na yalikuwa yanaonesha kuwa siona huo ugonjwa changamoto ni uzembe wa kunywa maji ya kutosha kwa maelezo ya daktari ...ndo nikapigwa na butwaaa na kubaki dilemma 😅

Je kipi ni kipi wakuu na niamini nini kwenye hili?

20211102_065243.jpg
 
Zamani ilikuwa Malaria, baadaye ikawa Typhoid na kwa sasa ni UTI. Yaani karibu kila mtu akienda kupima ataambiwa anazo, hata kama haumwi chochote. Hivi vituo binafsi vingi ni wizi mtupu.

Kwa uzoefu wangu mdogo sana, kwenye suala la vipimo vya maabara sio sahihi kwenda kupima kwenye hospitali binafsi, ni bora kwenda kwenye hospitali za serikali japokuwa huduma ni mbovu, majibu yanachelewa na uhuni ni mwingi lakini ni vigumu kwao kukupa majibu ya uongo kuwa unaumwa kitu fulani.
 
Duuh mbona nmekuwa disappointed, maana natumia dose ya UTI sku ya sita leo[emoji28]
 
Zamani ilikuwa Malaria, baadaye ikawa Typhoid na kwa sasa ni UTI. Yaani karibu kila mtu akienda kupima ataambiwa anazo, hata kama haumwi chochote. Hivi vituo binafsi vingi ni wizi mtupu.

Kwa uzoefu wangu mdogo sana, kwenye suala la vipimo vya maabara sio sahihi kwenda kupima kwenye hospitali binafsi, ni bora kwenda kwenye hospitali za serikali japokuwa huduma ni mbovu, majibu yanachelewa na uhuni ni mwingi lakini ni vigumu kwao kukupa majibu ya uongo kuwa unaumwa kitu fulani.
Kwa maoni yangu, kipimo cha kituo cha pili (yaliyosema hakuna UTI) huenda ndio sahihi zaidi.
 
Zamani ilikuwa Malaria, baadaye ikawa Typhoid na kwa sasa ni UTI. Yaani karibu kila mtu akienda kupima ataambiwa anazo, hata kama haumwi chochote. Hivi vituo binafsi vingi ni wizi mtupu...

Changamoto kweli mkuu ..yaani nimecheka njia nzima jana [emoji28][emoji28][emoji28]

Serikalini ule uvivu wa kusubiria ndo kunatufanya tuone hizi za private ni nzuri sema unachoongea ni ukweli mtupu
 
Kwa maoni yangu, kipimo cha kituo cha pili (yaliyosema hakuna UTI) huenda ndio sahihi zaidi.

Ata mimi niliamini kuwa ya pili ndo yanaweza kuwa kweli kwa ninavojisikia

Sema kuna somo nimelipata jana kubwa
 
UTI ili iwe clear mkojo unapandikizwa (culture) harafu ndiy wanapima kwa kutumia microscope .

Vipimo vingine vinavyopatikana kwetu uswahilini havina majibu sahihi.

Watu wanakimbilia kupima badala ya kumuona daktari akamueleza shida yako kwenye maelezo mazuri yana zaidi ya 75% ya kujua tatizo linalokusumbua, na kama maelezo yako yakaendana na tatizo dhahiri hamna hata haja ya kipimo unatibiwa na unapona

Kingine kinachowasumbua watu wadhanie wana uti ni unywaji wa maji na ulaji mbovu ambao unasababisha mkojo uwe very concetrated unasababisha irritation ya nerve za njia ya mkojo na kumsababisha mtu kuhisi maumivu

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Lee

Asantee mkuu ..
 
Wiki kadhaa nilikuwa nasumbuliwa na UTI baada ya kupata vipimo katika kituo cha afya X na doctor akanishauri nitumie dawa make alisema sio nyingi ni ya kawaida ..baada ya kumaliza dozi ikabidi nirudi...
Hizi sample za Mkojo hazifanani.
Seems kuna errors...
Sababu zinazonifanya nione kuna errors sample ya kwanza inaonesha una Kisukari ama una sukari kwenye Mkojo na sample ya pili inaonesha hamna sukari kwenye mkojo.

Inabidi ufahamu hizo printed results ni za Urine analyser haiwezi kukubambiki uongo.

Possible answers

Hawakuweka Label kwenye Mkojo wako wakauchanganya na Mkojo wa mtu mwingine...

Errors kama hizo huwa zinatokea
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Zamani ilikuwa Malaria, baadaye ikawa Typhoid na kwa sasa ni UTI. Yaani karibu kila mtu akienda kupima ataambiwa anazo, hata kama haumwi chochote. Hivi vituo binafsi vingi ni wizi mtupu.

Kwa uzoefu wangu mdogo sana, kwenye suala la vipimo vya maabara sio sahihi kwenda kupima kwenye hospitali binafsi, ni bora kwenda kwenye hospitali za serikali japokuwa huduma ni mbovu, majibu yanachelewa na uhuni ni mwingi lakini ni vigumu kwao kukupa majibu ya uongo kuwa unaumwa kitu fulani.
Kwa nini huende kupima wakati haumwi? [emoji3]
Watu wengi wanatembea na UTI, especially wanawake na wengine hawana dalili.
Kitu hiki uitwa Asymptomatic UTI.

Na wakati mwingine mpaka haishauriwi kila UTI kuitibu, especially mtu kama hana dalili hata moja, baadhi ya watu wanaweza tibiwa kama watoto, wajawazito na wenye kisukari au ambao Daktari ataona ni high risk
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Asantee mkuu ..
Mkuu hapo umechanganywa umepewa majibu sio yako
Mimi ni mtaalam wa afya
Check hayo majibu vzr
Majibu ya kituo X yanaonesha una UTI na kisukar
Majibu ya kituo Y yanaonesha huna hata kimoja

Mashine iliyotumika inaitwa urine analyzer kamwa haitoi majibu ya uongo never ever

Kwanza majibu ya kituo X hayaoneshi jina lako hukugungua hilo??

Kituo Y yanaonesha jina lako
Hao jamaa wamechanganya majibu
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Hebu tuanze moja, wewe unajisikiaje? Nini kimekufanya ukaenda hospitali.

Maana kwa hayo majibu huenda majibu ya kwanza ni sahihi.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Hizi sample za Mkojo hazifanani.
Seems kuna errors...
Yes ata doctor wa Y aliniuliza kama nina historia ya sukari nikamwambia sina na sukari yangu iko ok naye akawa na dukuduku na uwezekano wa kuchanganya majibu ...ila akaongeza kuwa mashine za upimaji nazo zinatofautiana japo na uzembe unachagiza
 
Hebu tuanze moja, wewe unajisikiaje? Nini kimekufanya ukaenda hospitali.

Maana kwa hayo majibu huenda majibu ya kwanza ni sahihi.
Mkuu nimeeleza wiki mbili zilizopita nilikuwa na UTI na nilipima katika hicho kituo baada ya kumaliza dawa ikabidi nirudi kupima kuona kama nimepona
 
Back
Top Bottom