Msaada makadirio kwa ramani hii

Habarini wakuu
Naombeni msaada wa makadirio ya tofali na material za ujenzi kwa ramani
View attachment 2100999
Nataka nikwambie wazi hii nyumba ni kubwa. Kama haujajipanga kisawa sawa basi ujipange.

Hapo andaa tofali 3,600, nondo za 12mm (makonde) tani moja na nusu, binding wire 10kgs, nondo za 6mm 20, Kokoto lori kubwa za 18m³ mbili, mchanga lori 3 za 18m³ na cement mifuko 300, hapo utakamilisha yote bila plasta na paa.
 
Du si mchezo kiongozi ni hatari ee!!.Ngoja nipandishe roofing plan tuone.

Asante Sana kwa mchanganuo.Nimechukua notes tayar
 
16 by 14 m ni nyumba kubwa sana.Gharama za ujenzi mpaka ikamilike ni kati ya Mili 48 hadi 90 kwa kutegemea location,fundi,materials na ubora wa kazi unaohitaji.
Asante kwa mchanganuo kiongozi.Kidogo umenipa matumaini.Sehemu nilipo material ni wastani hvyo naweza range kwenye hyo 90
 

Acha kumtisha hii ni nyumba ya wastan ila sio kubwa kihivyo kama unavyosema ,ingekua kubwa labda kama ingekua na sqm 300 na kuendelea,enewei hapo andaa 16m ,kukamilisha msingi hadi boma kukamilika,ukiona hauezi unaweza kuongea na fundi apunguze ukubwa kidogo wakati wa kuset msingi,ila ikikamilika hivi ilivyo utaenjoy zaidi nyumba itakua na space ya kutosha,sio vile vyumba ambavyo hata kabati ni ngumu kukaa.
 
Asante Sana kwa ushauri kiongozi.Naendelea kuchukua hatua Ili ni execute hii plan.
 
kwangu mimi hii nyumbani ni kubwa sanaa
1. ina kuta na kona nyingi so tegemea tofali nyingi kwenda hapo kati ya 3000-4000
2. mziki wa hiyo nyumba upo kwenye upauaji hapo kama hujajipanga kiukweli itakugharimu sana andaa sio chini ya 10-12 mill. na inaweza kuzidi.

kwa uzoefu mdogo mpaka kukamilika hii nyumba andaa 60-70 mill.

gharama pia haziewezinkuwa sawa kulingana na materials na maeneo uliopo... zinaweza kuzidi au kupungua......

ushauri....
kama ni ramani yako pendwa na unajiweza kiuchumi fata moyo wako ila kama upo kwenye kutathimini badili mawazo kama tu ni mtumishi/m.biashara wa kawaida na unafamilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…