Msaada. Makadirio ya kodi kutoka TRA

Msaada. Makadirio ya kodi kutoka TRA

ukisoma michango ya wanaJF unagundua wazi watu hawana elimu ya kodi, ila kama ilivyo kawaida yetu tunadhani tunajua kumbe ni kinyume. Jana nilikuwa ofisi za TRA nilienda kufanyiwa makadirio kwenye kibiashara changu kidogo. Muda nipo foleni nilishuhudia watu watatu wanalia. Wamekadiriwa kodi kubwa. Mimi naamini sivyo. Maafisa wa TRA wanakukadiria kodi kadri unavyojieleza. Ukienda kwake ukaropoka-ropoka kodi itakuwa kubwa. ni vizuri kama hujui mambo ya kodi, upate ushauri wa kitaalamu kabla hujaenda kuropoka na baadae kutoa machozi.
Cha msingi na kikubwa jitahidi kupata uelewa wa kodi, pitia kwenye website yao wameweka tax laws. Ukitaka interpretation, visit their offices.
Hata mimi ndio ninavyoelewa hivi.
 
Sawa mkuu. Hii ni nchi pekee ambayo ukiwa honest unapigwa fine. Mimi naacha hii biashara nitawapa sababu za kuacha sina sababu za kukaa chini kuwalalamikia watu wasio jielewa. Wao vichwa vyao ni kodi tu. Na sidhani kama manager wao anaweza kuwa na mentality tofauti.
Kwanini una give up kirahisi? Ukiacha ni wewe utakaekosa kipato,wale jamaa mishahara yao iko pale pale. Kawaambie hio kodi haiendani na mapato ya biashara yako.
Nikuulize swali, ulishajaza zile karatasi za tra na kusain(self assessment)?
Kama hujajaza na hujasaini chukua nyingine nenda Kwa mhasibu wa kawaida tu hata rafiki akujazie kulingana na maelezo yako zipeleke tra wakagonge mihuri tu ndio inavyotakiwa.
Kodi unajikadiria wewe wao wakiona haifai wake dukani kwako wajitidhishe sio wakatae wakati hata hawajui duka likoje ni kosa.
Halafu umesema unawalipa tra 60,000 ya pango, hii ni wht ambayo ni 10% hivyo uliwaambia Kodi yako ni 600,000 kwa mwaka?!
 
Chini ya mil 4 ni machinga, nenda kachukue kadi ua 20,000
Wakuu za leo.
Katika kupambana na maisha nikaamua kuanzisha duka la rejareja almaarufu la mangi mitaa ya hapa Mwanza.
Nikaenda TRA kusajili TIN bana jamaa wakakadiria kodi nilipe 250,000 kwa mwaka. Sasa yaani nimeshindwa hata cha kuongea nawaambia mimi kwa hii miezi miwili kwa siku hardly naweza pata 10,000. Ikiwa siku nzuri atleast naweza pata 15,000. Hapo hujatoa pango, umeme n.k, Kwa mwezi unaweza ishia na faida ya 50,000. sasa hii kodi ya 250,000 wameitoa wapi. Hafu wanasema mauzo yangu kwa mwaka ni mil 9.6 aseee nimejuta.
Sasa nimeamua kuachana na hii biashara bora nishinde nalala tu. Mtaji wenyewe laki 6.
Je. wakuu hii kodi 250,000 ni reasonable Kweli?
Hafu mbona kama wao wamekaa tu wanakukadiria ili ufeli ubaki na umasikini wako.
Nimeanza namna ya kuacha hii biashara, Kodi ikiisha tu naenda zangu kulima. Sasa ni namna gani naweza sitisha hili kadirio.
Asante
 
Pia vijana tujifunze kuwatumia watalaam ( Tax consultant), au vishoka

Wale.ni wazoefu , anaweza kudai 20,000 kama service lakini anajua jinsi ya kuongea.

Huyo aliyekwambia 250,000 hayupo serious ila anakaribisha mazungumzo ili umtoe kidogo.
 
eeh dawa ndio hiyo
 
Mkuu nachosema ndo icho. Nimekadiriwa turnover ya over 10m per year sasa mtaji wa 6/7 turnover ya 10m imetoka wapi?

Very possible, depending on the movement of trading stock. Don’t be fooled by the magnitude of capital, but by the volume of sales. One could have a capital of 600k but making sales in the region of seven digits per week. So it is from this volume of sales, presumptive tax is calculated.
 
Kwanini una give up kirahisi? Ukiacha ni wewe utakaekosa kipato,wale jamaa mishahara yao iko pale pale. Kawaambie hio kodi haiendani na mapato ya biashara yako.
Nikuulize swali, ulishajaza zile karatasi za tra na kusain(self assessment)?
Kama hujajaza na hujasaini chukua nyingine nenda Kwa mhasibu wa kawaida tu hata rafiki akujazie kulingana na maelezo yako zipeleke tra wakagonge mihuri tu ndio inavyotakiwa.
Kodi unajikadiria wewe wao wakiona haifai wake dukani kwako wajitidhishe sio wakatae wakati hata hawajui duka likoje ni kosa.
Halafu umesema unawalipa tra 60,000 ya pango, hii ni wht ambayo ni 10% hivyo uliwaambia Kodi yako ni 600,000 kwa mwaka?!

Njia nzuri ya kuepuka kukurupushana na TRA, keep records of your business, and try to be transparent. Issue manual receipt on every sales and retain the copies of the receipts. When you buy your trading stock, make sure you obtain a receipt which matches the amount of money you have paid. Keep record of all other expenses incurred during the year. Ikifika muda wa kwenda kukadiriwa beba mzigo wote wa record zako nenda kaubwage kwenye desk la ofisa anayekukadiria. If you are keen enough you will learn from the presumptive tax rates that if you keep records, you are liable to lesser tax than huyu asiye na kumbukumbu.
 
Kuna aina mbili za makadirio makadirio ambayo unafanyiwa na Tra kwa mtu binafsi (Presumptive Income), kigezo chake ni mauzo yapo chini ya millioni 100 na zaidi ya milioni 4.Kwa kampuni yaani limited company wao wanajifanyia wenyewe na mtu yeyote anayezidi millioni mia anaweza kujifanyia. Sasa ukiwa unafanyiwa kodi ni kutokana na jedwali hili hapa chini.
Rates of tax under presumptive tax System.

Under this system, tax payable is established based annual turnover shown by taxpayers records. In absence of complete records, annual turnover will be estimated based on the best judgment of the commissioner. The turnover bands and their tax rates are as stipulated below:

Annual turnoverTax payable when records are incompleteTax payable when records are complete
Where turnovers does not exceed Tshs 4,000,000NILNIL
Where turnover exceeds Tshs 4,000,000/= but does not exceed Tshs 7,000,000
Tshs 100,000/=
3% of the turnover in excess of Tshs 4,000,000/=
Where turnover exceeds Tshs 7,000,000/= but does not exceeds Tshs 11,000,000/=
Tshs 250,000/=
Tshs 90,000/= plus 3% of the turnover in excess of Tshs 7,000,000/=
Where turnovers exceeds Tshs. 11,000,000/= but does not exceed Tshs. 14,000,000/=
Tshs 450,000/=
Tshs 230,000/=plus 3% of the turnover in excess of Tshs 11,000,000/=
Where turnover exceeds Tshs 14,000,000/= but does not exceed Tshs 100,000,000/=
NA
Tshs 450,000/=plus 3.5% of the turnover in excess of Tshs 14,000,000/=

Ukitaka kujua zaidi utembelee tovuti ya tra Tanzania Revenue Authority - Income tax for individuals
Ila pia jifunze kutumia wataalamu kwenye maswala ya kodi ni rahisi kwako zaidi
 
Si ninaweza kuweka kwenye soft copy mfano ninataka niweke returns zangu kwenye mfumo wa Spreedsheet niziweke Google Drive

Kila siku nakuwa narekodi mauzo

How about that
Nunua hata counter book
Mfano umeanza biashara leo basi utakapouza page ya kwanza juu kabisa andika February then chini piga mistari yako mitatu kutengeneza kijumba cha tarehe, bidhaa uliouza, na chumba cha mwisho nia kiasi cha ulichouzia bidhaa
 
Shida iliyopo ni baadhi ya waajiriwa wa serikalini wanaamini wao ni wabarikiwa na wanajua mambo yote. Wanatoa majibu rahisi kwenye maswali magumu tena magumu kweli kweli. Nimeona bungeni na nimeona hata kwenye kufanya biashara
 
Kuna elimu ya kodi wanatuficha
Mtaji kuanzia 0- milioni 4 uwezi kukadiliwa kodi kwa kuanza ila utalipa malipo madogo kupata leseni isiyo kuwa na makadilio mpaka ikivuka malengo wakija kukagua kukuta umevuka mtaji uliowekwa.
Acha kupotosha mkuu, tofautisha mtaji na mauzo!!hiyo uliyozungumzia hapo ni mauzo ghafi kwa mwaka, ndio mtu hatozwi kodi kitu ambacho ni kigumu kuangukia kundi hilo, ni kama vile haiwezekani, yaani ukiwa na mauzo ya kuanzia 11,150 kww siku tayari umeshavuka kiwango hicho hivyo unatakiwa kulipa kodi!!huyo muuza machungwa tu anavuka kiwango hicho, sembuse mwwnye duka?!!
 
Si ninaweza kuweka kwenye soft copy mfano ninataka niweke returns zangu kwenye mfumo wa Spreedsheet niziweke Google Drive

Kila siku nakuwa narekodi mauzo

How about that
Inawezekana mkuu
 
Ni kweli ila kwa sababu wengi hawajui wanapewa.makadirio ya ovyo hata.mimi nilipopata mtaalamu ndio akanifungua macho.
Kitu muhimu ni kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi kitu ambacho wengi hawafanyi.
Sasa kwa biashara mpya, hizo records unazitoa wapi?!!kwani huyo ni mteja mpya ambaye ndio kwanza anaanza biashara!!japo kwa mfumo wa kodi wa TZ, ukisema kila record ya mauzo, uiweke inavyotakiwa nakwambia huwezi toboa hata siki moja, ndio maana wengi hukimbilia kwenye makadilio tu, wewe waulize wenye sifa ya VAT, wanavyopata tabu huko kwenye returns!tena hizi mashine za efd!!kifupi kwa nchi zetu hizi kodi inakuwa mzigo, kutokana na kushindwa kuongeza tax base, wanawakamua wale wachache wanaowafikia.
 
Mfanyabiashara unajikadiria kuna fomu ya assessment unavyojaxa ndivyo utakavyolipa
 
Sasa kwa biashara mpya, hizo records unazitoa wapi?!!kwani huyo ni mteja mpya ambaye ndio kwanza anaanza biashara!!japo kwa mfumo wa kodi wa TZ, ukisema kila record ya mauzo, uiweke inavyotakiwa nakwambia huwezi toboa hata siki moja, ndio maana wengi hukimbilia kwenye makadilio tu, wewe waulize wenye sifa ya VAT, wanavyopata tabu huko kwenye returns!tena hizi mashine za efd!!kifupi kwa nchi zetu hizi kodi inakuwa mzigo, kutokana na kushindwa kuongeza tax base, wanawakamua wale wachache wanaowafikia.
Hapa nazungumzia rekodi ya mauzo na matumizi yako, hata chakula unachokula wakati wa biashara ni matumizi, unapolipa usafi, umeme ni matumizi kama una usafiri mafuta unayoweka ni matumizi au hata kama huna gharama za usafiri unaotumia ni matumizi, vocha za simu bando za internet ni matumizi kuna orodha ndefu sana za matumizi ambazo wengi hawaziweki wanafikiri ni matumizi yao binafsi kumbe wanatumia kwa ajili ya biashara ndio maana wahindi wanalipa kidogo sisi tunafikiri wanatumia rushwa.
 
Back
Top Bottom