MSAADA: Mama mkwe amenifungulia kesi ya uharibifu wa Mali

Status
Not open for further replies.
Ubarikiwe Mkuu
Mie mpare Wa Mama wa kipare ni wa Tata Sana, kama hayo mashamba na unapokaa ni kwao, hata kama mmejenga na Mume wako, ni either ujitahidi muelewane na mume au uhame!

Ngumu Sana kukaa kwenye mashamba ya ukoo wa watu na wewe huelewani nao na hata mume wako hamkubaliani na karudi kwao, mtoto ni mmoja tu, kama hamuelewani mwaka mzima nini kina kuweka hapo?

Labda kama mashamba mmenunua na Mume wako, ila kama mmepewa na wakwe na wa naishi karibu, that is never health, mwenyezi Mungu akupe wepesi.

Hiyo kesi sio kitu, it aisha na Wala hakuna shida 'kama unachosema hapa ni ukweli'
Maana sioni mashiko ya mahakama kabisa, kwa sababu kesi ni nyepesi, kuna tatizo kubwa zaidi la ku solve, maana nyinyi ni maadui, na hata mumeo hayupo upande wako.
 
Direct nataka nikwambia fanya upatane na familia ya mumeo..wewe una tatizo ususani kwenye majibu na kumbuka hilo ni kosa kuvunja mlango kwa sababu ulizo ziandika,kuna kati ya miezi sita au mwaka jela na faini juu.

Kisaikoloji utetezu wako hauna mashiko bali utakukandamiza mbele ya pilato. Hili bomu lililo andaliwa juu ya mke, mwanamke kuwa juu ya kila kitu mpaka mnajisahau ujue msipo jielewa mtaelewa.

Umeomba ushauri na huo ndio wangu ukipenda chukua ukiona haufai waachie JF.
 
I know,maana walianza case ya Talaka ilivyofika kipengele Cha chumo la pomoja wakawithdral case na ndo baadae kifungua hii
Ukweli hapo hutakiwi
Wanakuona king'ang'anizi wanataka uondoke wabakie na nyumba
 
Pole sana Shem. Hayo ni Mapito tuu na Shukuru kwani unakomazwa. Zingatia sana alichosema kambitza hapo juu.
 
Niliposoma maelezo yako nimegundua yafuatayo:
1- Wewe ni mwanamke mjuaji na mpumbavu unaetaka kua juu ya mume wako.
2- Unamume mjinga ambae hana uwezo wa kusimama na kuongoza familia.
3- Mama wa mume wako ni shangingi la mjini lisilotamani kuona mwanae akipata mke kwa hofu ya kukatiwa mrija wa pesa za mahitaji yake.
4- Huyo sio mume wako kwasababu hakuna ndoa mlioifunga (ingawa sheria inakulinda kwasababu mmeishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita.
5- Mwisho nina imani kesi utashinda kwasababu sheria inakulinda ingawa utachelewa kuipata haki yako.
Pia ukishinda kesi jiandae kuishi maisha magumu ya vita shari na ushirikina.
Mimi nakushauri ondoka kwenye hiyo nyumba na ukaanza maisha mapya (kama nilivyo fanyaga mimi) na Mungu atakubariki
 
Usimtishe, tambua nchi inaendeshwa na mama. Wataingia wanasheria wa kike atajua hajui huyo mpare.
 
Yaa ni mashamba ya ukoo wao.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Serious komaa nao, kimbilia TAWLA faster watakusaidia ata ushauri chakufanya. Ukiona vipi nicheki nikuunganishe na wanasheria wa kike wakusaidie mawazo kwanza.
 
Yaa ni mashamba ya ukoo wao.

Unakuwaje na uadui na watu kwenye ardhi yao, na Mume wako yupo upande wao na bado unapambana?

Kama unaamini katika uzima na kujitafutia, we jipange na uhame hapo katafute maisha na mwanao.

Hapo watakuja kukudhuru tu, achana na vita za kijinga, Nyumba mmejenga na mumeo kwenye Mali ya watu, na wana kaa hapo hapo.
 
Ahsante Mkuu,wahataki reconciliation yoyote,so namwachia Mungu tu
Ni shetani tuu anawachanga kaa chini jirudi.hakuna linalo shindikana chini ya jua
Mimi nakuombea dua magumu yote yapite kwa usalama juu yako na wengine..
Moja § Uwezi kuomba au kupewa talaka hali hauja olewa!
Pili § Eneo la makazi ni baba mkwe wako hata kama alisema jua si lako wala huyo jamaa (chochote tegemea wenzio watabadili maandishi)..
 
Kuna kitu kinaitwa mchumo unauhakika jamaa kajenga nyumba mwenyewe...?
Soma maelezo ya mleta mada ndio utaelewa,tatizo lenu mnajifanya wana sheria mkija mahakamani mihemuko yote inaisha...Sheria sio hadith za bibi na babu yako.
 
mhn! kwa harakaharaka hapo ndoa kama hauna na kwa mazingira yaliyopo hakuna mwanamke anayeweza kukaa akatulia na huyo mwanaume kwakuwa mama kwanza mke baadaye! Mama hajawahi kumwachia kijana wake aende na mazingira ni kwamba kijana kuna jinsi ambavyo anamtegemea mama na mama kunajinsi ambavyo anamtegemea mtoto na inawezekana mtoto hajui ila mama anajua. pia inawezekana ipo siri ya familia ambayo huwenda unaweza kuwa unaadhiri mambo yao. kwa lugha ngumu ni kwamba kuna ndoa kati ya mama na watoto ( sio kwa kadri ya tendo la ndoa hapana bali ni mshikamano wa mama na watoto) hivyo familia hii ndoa hazitakaa zitulie vinginevyo ufahamu wa mwanaume umerudi.
yapo pia mazingira ya maendeleo na hasa uchumi yakawa tabu sana kiukweli hapo kwa sasa hakuna future ningekushauri utengane naye kwa muda ufanye yako kisha ipo siku kama bado mnapendana atarudi tu. vinginevyo ni kama unaoga maji mchana kweupe nje na maji yapo kwenye tenda huku unapambana watu wasikuone na pia maji yasiishe
 
Yes wote wapare
Pole wanyambo huwa wanauzuri fulani ambao sio ajabu mama mkwe kukuonea wivu, je ukijitafakari wewe unamakwazo gani kwa mumeo au huwa mumeo anakulalamikia mambo gani? Weakness zako zimkwazazo mumeo unazijua? Mume kukuhama nyumba ni big issue
 
inaonekana wamejenga nyumban kwa mume na mume hawalewan so hapo ht nyumba ukute ma mkwe anasema ni yakwake na kwakuwa imejengwa kwake hapo kuna mtihani
Ni kweli kuna mtihani hapo lakini Ushindi ni Lazima. Kama hatojali anaweza kuomba msaada kwa Ofisi ya Ustawi wa Jamii(W). Inaonekana pengine mama mkwe hampendi huyu mke wa mwanae na labda ameshamshawishi mwanae (Mume wa huyu mama) amwache kiaina. Yaani anataka waachane/kuwa-Achanisha/Kuwatenganisha.
La msingi ni kwa huyu anayeomba msaada awe mtulivu sana asiyumbe-yumbe katika kipindi hiki kigumu esp. kuanza kutafuta waume na mambo kama hayo au kuyumbishwa na ma-bush lawyers au wanawake wenzake kwa ushauri mbovu kabla kesi haijaisha.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…