Ningekuwa mimi Ningenunua Mark X kama uwezo wa kununua upo. Mark X ina ulaji mzuri wa mafuta kama ni mpya na inafanyiwa service vizuri. Uzuri wa Magari kuanzia Mwaka 2005 na kuendelea mengi yao hutumia Umeme sana kuliko Mafuta ulaji wa Mafuta wa Verosa cc1900 unalingana na Mark X ya cc2500. Wengi wetu tunasema gari flani linakula mafuta kwasababu wengi wetu tunaweka mafuta ya elfu 10 hadi kumi tano ukiendesha kidogo tu taa ishawaka hapo sasa unaanza da gari inakunywa mafuta hiyo..Verosa kiukweli Bodi yake sio kivile japo la mark x ni jepesi sana ila kimuonekano Mark X ndio gari kwanza ina comfortability, na ni nzuri kwenye lami ila offroad unaitesa na kuichosha tofauti na verosa inaweza kuhimili vishindo. Yangu ni hayo ngoja wengine waje waongezee na kurekebisha pale ambapo sipo sahihi
Unaeza nambia hizo gari za kwanzia 2005 zinatumiaje umeme mwngi kuliko mafuta😁😁