Msaada: Matumizi sahihi ya asali

Msaada: Matumizi sahihi ya asali

nyumbatatu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,076
Reaction score
939
Habari wanajamvi!, Ninafahamu kwa ujumla kuwa asali ni chakula na pia ni dawa. Lakini hapo kwenye kipengele cha chakula ndipo ninapohitaji ufafanuzi kwa maana ya matumizi sahihi. Kwani katika kukua kwangu nimetumia asali mara kadhaa kwa kulamba tu mpaka kikopo kinaisha, pia nimetumia asali kama mboga/kitoweo ili niweze kufurahia ugali wetu, pia nimetumia asali kama mbadala wa sukari kwenye chai. Je, katika matumizi hayo usahihi zaidi upo wapi na makosa yako wapi( na sababu zake), na kama kuna mutumizi mengine zaidi nilivyowahi kutumia napenda kufahamu. Nawasilisha.
 
Asali ni dawa, kama unayo akiba ya kutosha jitahidi kuitumia kwa utaratibu mzuri.
 
Tangu na tangu nilikua najua kuwa asali ni utamu utamu tu fulani basi.
Ila baadae nikasikia kuwa ni dawa.
Nami ningependa kujua ikiwa kama dawa inatumikaje?
 
Back
Top Bottom