nyumbatatu
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 1,076
- 939
Habari wanajamvi!, Ninafahamu kwa ujumla kuwa asali ni chakula na pia ni dawa. Lakini hapo kwenye kipengele cha chakula ndipo ninapohitaji ufafanuzi kwa maana ya matumizi sahihi. Kwani katika kukua kwangu nimetumia asali mara kadhaa kwa kulamba tu mpaka kikopo kinaisha, pia nimetumia asali kama mboga/kitoweo ili niweze kufurahia ugali wetu, pia nimetumia asali kama mbadala wa sukari kwenye chai. Je, katika matumizi hayo usahihi zaidi upo wapi na makosa yako wapi( na sababu zake), na kama kuna mutumizi mengine zaidi nilivyowahi kutumia napenda kufahamu. Nawasilisha.