Ndugu zangu naombeni msaada juu ya maumivu wakati wa haja kubwa hata baada ya kumaliza huwa napata maumivu yanayopelekea hata kushindwa kukaa,Na pia kuna kama nyama imechomoza kwa nje kwenye tundu la haja kubwa,Napata choo kigumu sana pamoja na jitihada za kula marunda na mboga za majani kila diku na Maji lita 4, je huu ni ugonjwa gani?Nifanyeje?
pole sana
ugonjwa huo unaitwa haemorrhoids hizi ni vericose vain zinakuwa kwenye m,kutokana na kutumia nguvu nyingi wakati wa kunya vinavimba,vingine vinapasuka,vingine vinakuwa ndani ya m,na vingine kwa nje ndo hivyo vinachomoza unapojisaidia.
mambo mengi yanayochangia ni kukaa muda mrefu,wakati wa mimba kutokana na uzito mwingi kuelekezwa chini,kubeba vituvizito.
........mambo ya msaada vizuri uendelee kunywa maji mengi,matunda,mboga sana kama ulivyosema ni msaada mzuri.
.........usiende haja kama unaona utahitaji kutumia nguvu kuutoa mzigo,subiri mpaka mzigo uwe umeiva sawasawa kwenda kulenga tundu tu la choo unashuka wenyewe bila nguvu.
..........mara nyingi vinaweza tokea halafu vikaisha vyenyewe tu.
...........kama vitaendelea muda mrefu nenda hosp.wakaangalie wanaweza kukupa dawa za kusaidia kukausha ama kufanyiwa band ligation yaani kile kinyama kinafungwa kwa kamba kwenye base yake kinakosa mzunguko wa damu mpaka kina kauka.ama
......kufanyiwa upasuaji mdogo kuviondoa.