Msaada: Mbwa wangu amebakiza saa machache afe

Pole sana majirani zako wanakuchukia kina kitu itakua umewakosea au Mbwa wako unawaacha hovyo
Hapana mkuu mbwa wangu huwa nawafungulia jioni kula ila asubuhi huwa nawawekea chakula humo humo kabla sijaondoka..
Huyu jirani yangu tulitofautiana kipindi fulani, mwanae alikuwa anamtongoza mfanyakazi wangu..
 
Hapo kwako kuna virus ambao wamewaathiri maini yao, inakuwa kama hepatitis kwa binadamu. mbwa wako watatoa dalili kama matumbo kujaa, kukojoa mkojo kama una damu vile, kunya kinyesi cheusi, miguu ya nyuma kukosa nguvu, kukonda ghafla, kukosa hamu ya kula, ukiona hizo dalili jua its too late, maini yao yamesha chakazwa, next time ukifuga hakikisha wakifika miezi mi nne nenda kwa bwana mifugo awachome chanjo ina chanjo za virus aina 4 au tano kwa pamoja kuzuia hayo magonjwa, hii haihusiani na chanjo ya kichaa cha mbwa.

Hata mm nilishawahi kuwaza ni sumu ila kumbe ni hii kitu, dozi zake ni hizi mbili, ila kuwa na uhakika muite bwana mifugo afanye post mortem ya mizoga


View attachment 1906439View attachment 1906440
 
Funga kamera za ulinzi hapo kwako na uweke katika maeneo ya siri sana hata watoto wako wasijue.

Halafu fuga mbwa wengine. Tena hawa wasasa hivi ikibidi wawe wanavuta bangi kabisa.


Mbaya wako akija tena utaweza mjua kwa haraka sana. Mimi naamini sana msaada wa technology zaidi kuliko matumizi ya mbwa maana mbwa ndio kama hivyo wanaweza malizwa chap na sumu kali.
 
Nashukuru sana mkuu
Unayosema karibu yote yamewatokea walikonda ghafla kwa siku moja tu.!
Lakini kwanini wafe wote ndani ya siku Moja?
 
Amina.

Hutakiwi kuishi kwa kuwakwaza wengine kiasi cha kupelekea wakuchukie namna hii.

Tubu dhambi zako, Na uwapende jirani zako kama unavyojipenda.
Una uhakika mimi ndio nimewakwaza?
Uwe unauliza mkuu wangu Dunia hii imejaa uhuni mwingi.
Jirani yangu huyo niliwahi kumpeleka mahakamani.. Alizidi kunifanyia uhuni
 
Pole sana mkuu, je, mbwa wako walipata chanjo zote? Wakati mwingine inaweza ikawa walipata maambukizi magojwa hasa ya virusi.

Najua inauma sana kupoteza mbwa ambaye ni rafiki na mlinzi wa familia.
Nashukuru siku nyingine nitafuatiia sana mambo ya chanjo
 
Mm nnavyopenda doggy Acha tu
Hpa nmeguswa sana
Ungewawahia daktari mapema

Ova
Ni kweli mkuu mbwa hawa pia walikuwa ni zaidi ya rafiki kwa sisi wapenda mbwa tunajua umuhimu wake

Pia walikuwa wananipotezea stress sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…