Msaada: Mbwa wangu amebakiza saa machache afe

Msaada: Mbwa wangu amebakiza saa machache afe

Mkuu, hiyo sio njia sahihi!
Pia, napenda kujua, hao mbwa ni wa aina gani?
Maanake hayo masikitiko yako, haionyeshi kuwa ni hawa MBWA KOKO wetu!
Koko alikuwa mmoja na hawa breed za kizungu wawili.
 
Yawezekana wakapata maambukizi ama ugonjwa, ila mazingira haya ya kufa watatu kwa kufuatana sio ugonjwa wa ini.

Hapa wangetofautiana sana muda wa kuumwa na kufa.

Hapa naona sababu pekee ni sumu.
 
Pole sana majirani zako wanakuchukia kina kitu itakua umewakosea au Mbwa wako unawaacha hovyo
Unajua figisu za uswaz?, kwanza ukimpenda na kumjali awe mbwa au paka watu wanamaind wanakuona unaringa
Sasa usiombee utoke na mbwa uende jogging hapo ndo watanuna hatari..

Pili mbwa anaona mambo meng sn usiku hvy mapilot (wanga) hawawataki kabisa utaona tu watakwambia hawa mbwa wako wanapiga sana kelele usiku hatulali!.. Jua tayari hapo sababu mbwa hawez kubweka bila sababu.
 
Dogii wangu alikufa mwaka jana, hadi leo sina, nilimpenda sana,
Natafuta dogii mwingine
 
Nyoka anauma mara Moja tu anaishiwa sumu. Asingeweza kuwauma wote watatu na kuwaachia sumu
Inategemea na aina ya nyoka ! Koboko anauma mara nyingi tu na zote zinakuwa na dose ya sumu.
Tabora huko koboko anaweza kingia kwenye banda na kupukutisha mbuzi kadhaa .
 
Pole sana ndugu kwa yaliyo kupata, naomba niseme kitu hapa.1 unasema Mbwa walipewa chakula na tunahisi ilikuwa sumu, nani huwa anawapa chakula? na huwa unawapia chakula nnje?2 Nyumba yako imezungushwa ua?3 Huwa unawafunguwa wote kwa pamoja wakati wa kulinda?

USHAURI:
1, Nakuomba usiwe unalishia chakula Mbwa nnje ya banda lao

2, Nakuomba kama Nyumba yako imezungushiwa ua usiwe unawafungulia Mbwa wote kwa pamoja, ukitoa mmoja ndani, 2 wabakie inakuwa rahisi mmoja akipewa sumu wengine watabweka mpaka utaamka tu, maana Mbwa wakiona hatari kuna mlio wanabadilika ufokaji lazima utaamka.

3, Mtu wa kuwalisha awe mmoja ikiwezekana na wakati muupangilie itawasaidia kutokula hovyo.

4, Mbwa uwe unawatarishia chakula kuwapikia maana cha kuchukuwa hotelini huwa ni hatarishi kwa ulaji wa Mbwa maana anapata harufu nyingi tofauti.

5, Ukiwa na nafasi unaweza kusimamia mwenyewe kumwongoza Mbwa asile vyakula vya kuotoka chini, ni somo rahisi sana hilo.
Kwaleo tuishie hapo kwanza. Mbarikiwe nyote. 🙏
 
Kuna Virus wanaitwa PARVO ndio dalili zake hizo,mie last week nimezika mbwa wawili waliokikufa kwa interval ya week moja,wanatakiwa wapate chanjo mapema,ugonjwa huu ukimpata mbwa kupona ni bahati sana
Kuna uzi wa mwaka 2019 unazungumzia huu ugonjwa hapa jfView attachment 1906903
 
Back
Top Bottom